Kuna baadhi ya wanaume wana ndoto siku moja wawe na uwezo wa kumuoa mtoto wa Rais wa Marekani aitwaye Malia Obama, lakini swali je ni kweli itawezekana? Mmoja mwenye ndoto kama hiyo ni wakili
kutoka Kenya ambaye amesema atajitoa kwa
kila hali kuhakikisha anatimiza ndoto zake za kuweza kumpata mtoto huyo huku akimuahidi Rais Barack Obama vitu mbalimbali kama mahari kwake.
kila hali kuhakikisha anatimiza ndoto zake za kuweza kumpata mtoto huyo huku akimuahidi Rais Barack Obama vitu mbalimbali kama mahari kwake.
Kiprono Matagei amesema yupo tayari kumzawadia rais huyo ng’ombe 50, kondoo 70 na mbuzi 30 ili ampe mtoto wake Malia ambaye kwa sasa ana miaka 17.
Amesema alianza kumpenda mtoto huyo
tangu mwaka 2008 wakati akiwa na miaka 10 na alikua akisubiri apate
nafasi hiyo, na sasa anatumia mwanya wa Rais huyo atakapofanya ziara
nchini humo mwezi ujao ili aweze kuongea naye.
Amesema familia yake imeridhia kumsaidia
kufanikisha kumpata mtoto huyo kwa kuchangia gharama za mahari
aliyoahidi kumpa Rais huyo.
No comments:
Post a Comment