Mshambuliaji wa kimataifa wa uingereza Daniel Sturridge amesema upasuaji wa nyonga uliofanyika leo kule nchini Marekani umefanikiwa na anatarajia kupona haraka na kurudi katika majukumu yake ya klabu ya Liverpool.
Mshambuliaji huyo alikutana na jopo la madaktari bingwa nchini marekani baada ya kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara msimu huu na kumfanya akose michezo mingi sana ya timu yake ya Liverpool na timu ya taifa.
Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea alipost katika ukurasa wake wa instagram kwamba ”nahitaji kuwajulisha wote kwamba upasuaji umeenda vizuri na napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kuliwezesha hili” Aliandika katika ukurasa huo
No comments:
Post a Comment