06 May, 2015

Emanuel Adebayor ameandika maneno mengi sana kwenye page yake ya Facebook kuhusu matatizo yake na familia.

ADE
Emanuel Adebayor ameandika maneno mengi sana kwenye page yake ya Facebook kuhusu matatizo yake na familia. Kitu cha msingi alicho kisisitiza ni kwamba hajaandika kwa ajili ya kuaibisha familia yake lakini anataka kuwaonyeshea mfano na familia nyingine zijifunze.

Adebayor “SEA” anasema ameziweka hizi story kimya muda mrefu lakini hivi sasa ameamua kuziweka wazi. Anaamini matatizo ya kifamilia yanaweza kuwa solved ndani lakini anaweka wazi ili wengine wajifunze.
Wakati ana miaka 17 ndio alianza kupata mshahara wa kwanza kama professional footballer na alitumia pesa zake kujenga nyumba kwa ajili ya familia yake. Mwaka 2008 alivyoshinda tuzo ya African Player of the Year alienda na mama yake kwenye jukwaa na kumshukuru kwamba bila yeye asingefikia hayo mafanikio.
Mwaka huo huo alimpereka London kwa ajili ya matatibabu na binti wa Adebayor alipozaliwa alimpigia simu mama ake kumwambia , mama akakata simu na hakutaka kusikia chochote kuhusu hilo.
Kuna muda alimtumia pesa mama ake aende kwenye maombi kwa T.B Joshua akae Nigeria kwa muda wa wiki moja lakini alikaa siku mbili na kuondoka. Nilipigiwa simu kwamba mama ameondoka Nigeria nje ya muda tuliokubaliana.
Zaidi ya hapo nilimpa pesa za kuanzisha biashara ya cookies na vitu mbalimbali na nikawaruhusu watumie picha yangu na jina langu kwenye hizo bidhaa. Kitu gani kingine mtoto anaweza kufanya kwa mzazi kilicho ndani ya uwezo wake.
Miaka michache iliyopita nilimnunulia nyumba huko Ghana kwa gharama ya $1.2 milion, nikamruhusu dada mkubwa akae humo ndani na pia half brother anaitwa Daniel akae kwenye hiyo nyumba. Baada ya miezi michache nikiwa likizo nikaenda kwenye hiyo nyumba nikakuta nyumba nzima imepangishwa na dogo Daniel kafukuzwa.
Nilimpigia simu kumuuliza kwanini kafanya hivyo nikaambulia matusi kwa muda usiopungua dakika 30 kupitia simu. Nilivyompigia simu mama na yeye alifanya hivyo hivyo. Huyu ni dada yangu ambae kila kitu anachofanya leo kwenye biashara na magari anayoendesha yametoka kwangu.
Kaka yangu Kola alikua ujerumani kwa miaka 25, alisafiri nyumbani Togo mara 4 kwa gharama zangu na mimi nalipia gharama zote za watoto wake pamoja na elimu yao. Wakati niko Monaco alikuja kuniomba kiasi cha pesa kuanzisha biashara, mungu pekee anajua kiasi gani nilimpa.
Kaka yangu Peter alivyofariki nilimtumia Kola pesa za kutosha kuja Togo kwa ajili ya msiba lakini hakuja. Baadae akaanza kusema mimi nahusika na kifo cha Peter. Huyo huyo Kola ndio alifanya interview na The Sun ili apewe pesa na kusema story za uongo bila kujali inaniharibia mimi kaisi gani kwenye kazi yangu.
Familia pia iliwai kuandika baria kwenye Real Madrid kwamba eti nifukuzwe na klabu. Nikiwa Monaco nilijua ingekua vizuri kumsaidia mdogo wangu Rotimi kuingia kwenye academy ya soka ndani ya Ufaransa. Ndani ya miezi michache kati ya wachezaji 27 aliwaibia simu zao wachezaji 21.
Siwezi kusema kitu chochote kibaya kuhusu kaka yangu Peter ametangulia mbele ya haki. Dada yangu Lucia anaendelea kuwambia watu kwamba baba yangu ameniambia kwamba nisimpeleke Ulaya, Sababu ya yeye kuja Ulaya ni ipi?.Kila mtu yupo huko kwa sababu.
Nikiwa Ghana nikapokea simu kwamba ndugu yangu Peter anaumwa sana. Nikaendesha gari haraka ndani ya masaa 2 hadi Togo. Nilipofika nikazuiwa kuingia na mama, kitu pekee nilichoambiwa ni kwamba nitoe pesa na niondoke. Kiasi nilichompa mama mungu anajua.
Mwaka 2005 niliitisha kikao cha familia kumaliza haya matatizo na waliniambia nimjengee kila mtu nyumba na pesa kila mwezi. Hivi sasa Napata wakati mgumu kwenye foundation yangu, kila nikifanya kitu wanafamilia wananiambia ni kwanini nasaidia watu na kutumia pesa nyingi. Hii ni moja ya sababu kwanini foundation yangu imechelewa sana kuanza.
Nimeandika haya yote kutoa mfano tu kwa familia nyingine na sio kuiabisha familia yangu
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu DunianI - FIFA, Joseph “Sepp” Blatter ametuma salamau za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi kufuatia klabu ya Young Africans kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015. Katika salamu hizo za Blatter, amemuomba Rais wa TFF kufikisha salamu zake za pongezi kwa klabu ya Young Africans, wanachama, wapenzi wa mpira wa miguu kwa kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi mwakani katika michuano ya kimataifa barani Afrika. Blatter amesema anatambua mafanikio hayo ya kutwaa Ubingwa, yametokana na na jitihada za uongozi, wachezaji, bechi la ufundi, madaktari, wanachama , washabiki na kila mmoja aliyeshiriki katika kufanikisha kutwaa Ubingwa huo. Mpira wa miguu unapata mafanikio makubwa kwa kuvuka mipaka hadi kuwa kichochezi halisi cha maendeleo, unawasaidia wachezaji wa ngazi zote kuinua vipaji vyao na mbinu katika kuelekezwa na kubadilika wakati huo huo wakiwa wakiwa na nyoyo za ushirikiano. Aidha Blatter amesema mpira wa miguu kwa sasa ni shule kwa maisha, vijana wa leo wanaweza kufaidika kupitia kucheza mpira wa miguu kwa ngazi ya kijamii na mtu mwneyewe binafsi, ndio maana amewapa salamu za pongezi Young Africans na kuendeleza kazi yao na kuongoza njia ya mafanikio. Kujituma kwa klabu ya Young Africans kumewasaidia kushinda Ubingwa huu ikiwa ni ni mara ya 25, huu ni ushindi mkubwa katika mpira wa miguu.

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2015/05/sepp-blatter-aipongeza-yanga-kwa-kutwaa.html
Copyright © saluti

Copyright © saluti 5

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...