Yanga ambao mpaka sasa
wamebakiza mchezo mmoja kuhitimisha ratiba ya
ligi kuu Tanzania bara,
ikitokea wakapata ushindi watakuwa wamefikisha jumla ya pointi 55 ambazo
haziwezi kufikiwa na mabingwa watetezi Azam wala timu nyingine yoyote.
Katika mchezo wa leo katika Uwanja wa Taifa Dar, YANGA imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Maafande wa Ruvu Shooting, mchezo huu ulionekana kuchezwa upande mmoja, huku Ruvu Shooting wakionekana kuzidiwa kila idara na kuwapa nafasi washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Msuva kutawala mpira kwa kiasi kikubwa.
Yanga walianza kupachika magoli dakika ya 13 kupitia kwa Simon Msuva ambaye alifunga kwa kichwa akiunganisha krosi safi ya Niyonzima kabla ya Sherman kupachika goli la pili.
Dakika ya 45 kabla ya kwenda mapumziko Msuva tena akawainua mashabiki wa Yanga kwa kufunga bao la tatu.
Katika kipindi cha pili Tambwe alianza tena kuwainua mashabiki wa Yanga dakika ya 58 kwa kufunga bao la nne baada ya mabeki wa Ruvu kujichanganya na yeye kumalizia shuti.
Dakika ya 67 Sherman anahitimisha ushindi mnono kwa Yanga kufuatia likiwa ni bao la tano kwa kichwa krosi nzuri ya Abdul Juma.
No comments:
Post a Comment