WEKUNDU wa Msimbazi wamesahau
kipigo cha 2-0 walichopata mwishoni mwa juma katika mechi ya ligi kuu
Tanzania bara iliyopigwa uwanja wa Sokoine Mbeya dhidi ya wenyeji Mbeya
City fc.
Baada ya kucheza mechi 20 Simba
ilitangaza kushinda mechi 6 zilizosalia na tayari wameshapunguza mbili
ambazo walishinda 2-1 dhidi ya Kagera Sugar uwanja wa CCM Kambarage na
nyingine walipoteza Mbeya.
Katika hesabu zao, Simba wamebakiwa na mechi nne tu ili kumaliza msimu huu na mechi hizo ni:
Simba v Mgambo (Inachezwa kesho Uwanja wa Taifa )
Simba v Ndanda fc uwanja wa Taifa
Simba v Azam fc Uwanja wa Taifa
JKT Ruv v Simba Uwanja wa Taifa
Kocha mkuu wa Simba, Mserbia
Goran Kopunovic anaaendelea kukinoa kikosi chake katika uwanja wa Chuo
kikuu cha Dar es salaam (UDSM).
Katika mazoezi ya jana, vijana walionekana kuwa na maorali.
Kopunovic alisema: “Tunatumia
kipigo cha Mbeya kujiandaa na mechi zijazo. Ligi ina ushindani sana,
mechi za Simba ni ngumu, timu zinajipanga sana zinapocheza na Simba,
lakini mimi na Matola (Seleman) tunajitahidi kuimarisha kikosi kila
siku”.
“Mechi ya Mgambo ni changamoto nyingine, walitufunga kwao (2-0), lakini muda wa kupindua matokeo umefika”.
No comments:
Post a Comment