14 April, 2015

WAJUE WACHEZAJI HAWA WANAOTESA ULAYA ILA ASILI YAO NI AFRICA

1Mario Balotelli
Mario Balotelli anacheza mechi za kimataifa na the Azzurri na amefanikia akufunga mara 13 kwenye mechi 33 alizocheza. Mambo haya angeweza kuyafanya akiwa na timu ya taifa ya Ghana kwa sababu wazazi wake ni wazawa wa nchi hiyo.
ronaldoRolando
Ni beki mwenye kipaji na ameitumikia vizuri timu ya Ureno, lakini alizaliwa Africa nchini Cape Verde lakini alihamia Portugal akiwa na miaka 14 na mwaka 2006 akawa mwananchi kamili wa huko.steve mandanda
Steve Mandanda
Goli kipa wa timu ya taifa ya Ufaransa ambae alikua kwenye kikosi cha kombe la dunia mwaka 2010 pamoja na michuano ya Ulaya mwaka 2008 na 2012. Kama angeamua kuitumia nchi yake ya uzawa basi angekua golikipa wa Congo. Steve alichezea club ya Marseille na kwenye kuchagua timu ya taifa akachagua France.
naniLuis Nani
Huyu jamaa amezaliwa Cape Verde lakini ameiwakilisha vema timu ya Portugal. Hivi sasa yupo kwa mkopo kwenye club ya Sporting akitokea Manchester united. Nani ameshafunga magoli 15 akiwa kwenye timu ya taifa ya Portugal akiwa ndani ya mechi 83.angeloAngelo Ogbonna
Beki huyu wa Italy amezaliwa Cassino huko Italy lakini asili ya wazazi wake ni Nigeria. Ogbonna alikuana nafasi ya kuchagua kuchezea timu ya Nigeria au Italy lakini yeye alichagua nchi aliyozaliwa ambayo ni Italy.boatenbgJarome Boateng
Pacha wake amechagua kucheza timu ya Ghana lakini yeye ameamua kuchezea timu ya Ujerumani. Boateng mama yake ni mjerumani na baba yake ni mghana, kwahiyo pacha mmoja kachagua kucheza Ghana na Jarome anachezea Ujerumani lakini alikua na nafasi ya kuchezea Ghana.mutundi
Blaise Matuidi
Mchezaji wa kimataifa wa France alikua na nafasi ya kuchagua kucheza Angola au France. Baba yake ni raia wa Angola na mama yake ni raia wa France. Midfielder huyu akachagua kucheza kwenye timu ya France.
kherida
Sami Khedira
Huyu jamaa alikua na uwezo kabisa wa kucheza kwenye timu ya taifa ya Tunisia badala ya Ujerumani. Khedira amefanikiwa kwenye soka la kimataifa akiwa na Ujerumani kwa kushinda kombe la dunia mwaka 2014.
welbDanny Welbeck
Mapanki na yeye alikua na uwezo wa kucheza timu ya taifa ya Ghana lakini ameamua kucheza timu ya taifa ya Uingereza. Jina lake kamili ni Daniel Nii Tackie Mensah Welbeck na wazazi wake wote wawili ni raia wa Ghana.benzemaKarim Benzema
Karim Benzema alisema kwenye radio kwamba Algeria ni wazazi wake na nchi hiyo ipo kwenye moyo wake lakini kwa upande wa soka atacheza Ufaransa. Karim ana asili ya Algeria lakini anacheza timu ya taifa ya Ufaransa.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...