Mshindi wa tuzo ya Grammy
mwanamuziki Cornell Haynes ama kwa jina maarufu Nelly amekamatwa na
shtaka la mihadarati baada ya polisi kusimamisha basi alilokuwa
akisafiria mjini Tennessee nchini Marekani.
Alikamatwa kwa kuwa basi hilo halikuwa na vibandiko halali kabla ya kuchunguzwa kutokana na harufu ya bangi iliokuwa ikinuka.Idara ya usalama na usalama wa nyumbani baadaye ilisema kuwa Nelly alipelekwa hadi Jela ya kaunti ya Putnam baada ya basi hilo kusimamishwa.
Msanii huyo wa muziki wa kufokafoka alishtakiwa na makosa ya kumiliki bangi kabla ya kuachiliwa kwa dhamana .
Mtu mwengine ambaye pia alikuwa akiabiri basi hilo alikamatwa na kushtakiwa ,mamlaka imesema.
No comments:
Post a Comment