19 April, 2015

Ubaguzi dhidi ya wageni nchini Afrika kusini


Maafisa zaidi wa polisi wametumwa katika maeneo yenye mashambulio dhidi ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini.
Yamkini watu sita wameuawa na makundi yenye silaha, ambayo yanawalaumu wahamiaji wa kiafrika kwa kuchukua kazi zao nchini Afrika Kusini.
Rais Jacob Zuma amewatembelea watu hao walioathirika na ghasia hizo, mauwaji pamoja na kuibwa kwa mali zao huku akiahidi kukabiliana vilivyo na wimbi la mashambulio hayo.
Bwana Zuma alifutilia mbali ziara yake nchini Indonesia, ili kukabiliana na vurumai hizo zilizoanza majuma mawili yaliyopita.
Yamkini watu sita wameuawa na makundi yenye silaha, ambayo yanawalaumu wahamiaji wa kiafrika kwa kuchukua kazi zao nchini Afrika Kusini.
Nchini Harare Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, alilaani ghasia hizo.
Ghasia hizo zilianza baada ya mfalme mmoja wa Kizulu, Goodwill Zwelethini, kusema kuwa raia wa kigeni sharti waondoke Afrika Kusini.
Akiongea katika kambi hiyo iliyoko mjini Durban kiongozi mkuu wa jimbo la Gauteng, David Makhura, anasema kuwa uhasama na ghasia hizo zinazoshuhudiwa, haundamani na uhuru wa miaka mingi ambayo Afrika Kusini ilipigania

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...