
Msanii wa muziki wa
Bongo Fleva ambaye anaendelea kubaki kwenye kilele kila siku,
Nasib Abdul aka
Diamond Platnumz amejitolea kuwalipia wakazi 200 wa
Tandale Bima ya afya itakayo wafanya watibiwe bure kwenye hospitali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram
Nasib ameandika haya "
...Shukran
nyingi ziwafikie Edgepoint Company Ltd kwa kujitolea kunipa Bima ya
Afya kwa wakazi 200 wa Tandale, Bima hiyo ambayo itawaruhusu Wakazi hao
kutibiwa bure Hospitalini kwa Kipindi cha Mwaka Mzima bure...bima hizo
100 zitaenda kwa Watoto wa shule ya Tandale Magharibi, 50 kwa wakina
mama wajane wa Tandale na 50 kwa watoto yatima wa Tandale...Lengo na
dhumuni langu si kusaidia Tandale tu, lakini kwakuwa Mwanzo ni mgumu kwa
sasa naanzia Tandale ila naamini Wilaya na mikoa Mingine nitafika
ku#PushMtaa..."
Mawerenewz.blogpot.com ndio mtandao wako wakipekee
unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO,SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA
pamoja na KITAIFA
Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3,
facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>Zawadi_mawere.
AKSANTE.
No comments:
Post a Comment