26 April, 2015

TUNAJIFUNZA NINI KWA MBEYA CITY?

DSC_01971
  Timu hiyo inayomilikiwa na Manispaa ya jiji la Mbeya, ilianzishwa rasmi mwaka 2011 na miaka miwili baadaye ilifanikiwa kupanda ligi kuu. Ilikanyaga busati la ligi kuu msimu wa 2013/14 .
Ingawa ilikuwa ni timu ngeni lakini ilimaliza ikiwa nafasi ya tatu ikiwaacha wakongwe wa ligi hiyo Simba SC nafasi ya nne. Azam waliibuka mabingwa na
Yanga nafasi ya pili.
   Lakini msimu huu wa 2014/15 , wakali hao wa nyanda za juu kusini walianza vibaya ligi hiyo na watu wengi kuitabiria kushuka daraja.
   Mbeya City , wamecheza mechi 24 lakini wameshinda mechi 7 tu huku wakienda sare mara 10 na kufungwa mechi 7.
   Kiukweli baada ya kuonesha upinzani mkali mwaka jana , timu hiyo haikufanya usajili mkubwa zaidi ya wachezaji wachache kama Themi Felix na beki kisiki Juma Nyoso. Iliwaamini zaidi ya 90% ya wachezaji iliyo anza nao.
  Somo kubwa kwa Mbeya City ni uvumilivu juu ya kocha licha ya matokeo mabaya mwanzoni.
   City, imeburuza mkia mara kadhaa na kujikuta ikihaha kutafuta pointi za kubaki ligi kuu.
Lakini kaka yangu mzee Mwambusi na uongozi mzima wa halmashauri wamesimama kidete kuinusuru timu hiyo isishuke daraja.
  Kwa sasa wapo nafasi ya nne wakiwa na pointi 31 na wamebakiza mechi 2 dhidi ya Polisi Moro na Prisons.
  Ukiangalia matokeo ya mechi 6 za awali , City wamepoteza na kufungwa . Hii imewanyima mtaji wa kusaka ubingwa.
Mbali na kufungwa huko ni Yanga pekee waliofanikiwa kuwafunga idadi kubwa ya magoli. 6_2 kwa jumla ya mechi zote mbili.
   Tujifunze kuwavumilia makocha. Kuna wakati timu inafungwa si kwa uwezo mdogo wa kocha mbali ni sababu nyingine ambazo kwa namna moja ama nyingine zinazorotesha msingi mzima wa ushindi.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...