Miaka saba iliyopita mwanasoka mkongwe na staa wa mitindo duniani David Beckham na mkewe Victoria walirudia viapo vya ndoa yao, walisafiri na kuamua kufanya sherehe yao jiji la Marrakech, Morocco.
Ndoa yao ni mfano wa kuigwa kwa mastaa wengi duniani, imedumu kwa mrefu na mpaka sasa na watoto wanne.Safari hii mwanasoka huyo ambaye atakuwa na sherehe ya kutimiza miaka 40
siku ya May 2 2015 mwaka huu amepanga kwenda kusherehekea siku yake
hiyo pamoja na familia yake na washkaji zake wa karibu ndani ya Morocco, kulekule ambako ambako walienda kurudia kiapo cha ndoa yao.
No comments:
Post a Comment