27 April, 2015

Thierry Henry ameikosoa sera ya usajili ya Arsenal ya hivi karibuni

28080E2600000578-0-image-m-17_1430085416130
Thierry Henry ameikosoa sera ya usajili ya Arsenal ya hivi karibuni na ameitaka klabu yake hiyo ya zamani kununua wachezaji wa wanne wa kiwango cha juu majira ya kiangazi mwaka huu.
Mfaransa huyo anaamini kuwa Arsenal inahitaji golikipa, beki wa kati, kiungo mkabaji na mshambuliaji kama wanataka kushinda kombe la ligi kuu England.
Akizungumza baada ya suluhu ya jana ya Arsenal dhidi ya Chelsea, Henry, amemshambulia Olivier Giroud akidai kuwa The Gunners wataendelea kuhangaika kutafuta ubingwa kama Mfaransa huyo mwenzake ataendelea kuwa mshambuliaji chaguo la kwanza.
“Nadhani wanahitaji kununua wachezaji wanne-bado wanahitaji golikipa, kiungo mkabaji na nina wasiwasi wanahitaji wachezaji wa juu, wanahitaji mshambuliaji wa kiwango cha juu kama wanahitaji kuchukua ubingwa tena”.
“Tuna mfano mzuri wa Chelsea. Walikuwa wanahangaika kushinda kombe msimu uliopita. Waliingia sokoni walimnunua [Thibaut] Cortouis, [Nemanja] Matic, Cesc [Fabregas] na [Diego] Costa, sasa mambo ni mazuri”.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...