06 April, 2015

SIMBA YACHAPA KAGERA SUGAR BAO 2--1

ajib kageraKlabu ya Simba SC leo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya wenyeji wao Kagera Sugar katika mtanange uliopigwa kwenye uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Simba ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kunako dakika ya 49 kipindi cha pili kupitia kwa Ramadhan Singano kabla ya Kagera kusawazisha kupitia kwa Rashid Mandawa.
Mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib aliipachikia timu hiyo goli la pili na la ushindi kwa mkwaju wa penati, Kufatia ushindi huo Simba inakuwa imefikisha pointi 35  baada ya kucheza michezo 21.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...