‘Tanzania na Uganda zimepangwa kwa mara ya tatu kukutana katika hatua ya mchujo ya katika misimu mitano ya michuano ya CHAN.’
Ukanda wa CECAFA
Tanzania v Uganda
Djibouti v Burundi
Ethiopia v Kenya
Sudan wanavuka bila upinzani
KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Uganda (Cranes), Micho Sredojevic, amesema atakuwa na kikosi kipya kwa ajili ya michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN). Rwanda ni mwenyeji wa fainali za michuano hiyo mwakani.
Uganda imepangwa tena kwa mara ya tatu kuanza dhidi ya Tanzania (Taifa Stars) katika hatua ya mchujo wikendi ya Juni 21 mwaka huu. Uganda itasafiri kuija Tanzania katika mechi ya kwanza kabla ya kurudiana jijini Kampala, Uganda Julai 3-5.
Micho amesisitiza kuwa wachezaji wengi wa Tanzania waliocheza CHAN iliyopita, bado wanacheza nyumbani, hivyo hawezi kuwategemea wachezaji wachache wa Cranes waliokuwamo katika CHAN iliyopita kwa kuwa wengi wao sasa wanajiona ni wenye weledi huku hawako fiti.
“Tunahitaji kuandaa timu mpya. Ninaamini tukiwa na maandalizi mazuri, tunaweza kuing’oa Tanzania ambayo wachezaji wake karibu wote waliokuwamo katika kikosi cha kuwania kufuzu AFCON iliyopita, badi wanacheza ndani ya Tanzania,” Micho amekaririwa na mtandao wa Kawowo Sports wa Uganda.
No comments:
Post a Comment