Hili pambano ni kama dunia nzima inalisubiri kwa hamu yani.. vyombo vya habari vimelipa promo kubwa kiasi cha kwamba hata ambao hawafuatilii ndondi imebidi wafuatilie hawa jamaa ni akina nani hasa !!
Jana nilikusogezea pichaz zikionesha Manny Pacquiao akiingia zake Las Vegas na msafara kabisa wa pikipiki, basi kubwa na gari nyingine zikimsindikiza.
Leo ni zamu ya Floyd Mayweather ambaye ametumia muda wake kwenda kukagua ukumbi wa MGM Grand ambao utatumika kwa pambano lao.
Ukumbi ulifurika mashabiki.. camera za mapaparazzi nazo hata hazikuwa mbali.
Pambano hilo linatajwa kuwa pambano la
kifahari zaidi duniani na ambalo viingilio vyake ni vikubwa
ukilinganisha na mapambano mengine yaliyowahi kufanyika duniani.
No comments:
Post a Comment