‘Mtibwa na JKT Ruvu zilitoka
sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza ya VPL msimu huu iliyochezwa Uwanja
wa Azam jijini Dar es Salaam.’
MABINGWA wa Tanzania Bara 1999
na 2000, Mtibwa Sugar FC, wamepoteza mechi yao ya kwanza nyumbani msimu
huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kwenye Uwanja wa Manungu,
Turiani mkoani Morogoro baada ya leo kupigwa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu
Stars.
Bao pekee la kujifunga la beki
wa kati Andrew Vincent, limetosha kukisogeza kwa nafasi moja kikosi cha
Fred Felix Minziro kutoka nafasi ya 11 hadi ya 10 katika msimamo wa ligi
kikiishusha Coastal Union FC kwa nafasi moja.
Kocha mkuu wa Mtibwa Sugar FC,
mzawa Mecky Mexime, aliyewahi kuwa nahodha wa Taifa Stars na Mtibwa
katika enzi zake za kusakata soka, amesema baada ya mechi kuwa ubora wa
kipa wapinzani wao aliyeokoa mashuti mengi ya wenyeji.
Mtibwa wameendelea kubaki
nafasi ya saba katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi 28 sawa na Stand
United, Mgambo Shooting, JKT Ruvu na Coastal Uniuon zinazokamata nafasi
za 8-11.
No comments:
Post a Comment