16 April, 2015

Majibu ya DNA Test Aliyoifanya NAY WA MITEGO Kubaini Kama Mtoto Aliyezaa na SIWEMA ni Wake Ama Laa Yametoka..Majibu Haya Hapa


Image result for NAY WA MITEGONay aliingia kwenye utata huo takriban mwezi mmoja uliopita baada ya kupishana kauli na Siwema ambaye alimfumania akiwa na mwanaume mwingine nyumbani kwake, jijini Mwanza na kuamua kumchukua mtoto kisha kuishi naye jijini Dar kwa msaada wa mama yake mzazNay aliingia kwenye utata huo takriban mwezi mmoja uliopita baada
ya kupishana kauli na Siwema ambaye alimfumania akiwa na mwanaume mwingine nyumbani kwake, jijini Mwanza na kuamua kumchukua mtoto kisha kuishi naye jijini Dar kwa msaada wa mama yake mzazBaada ya utata mzito kutawala kwenye vyombo vya habari juu ya uhalali wa mtoto wa Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa mzazi mwenzake Siwema Edson, hatimaye kipimo cha vinasaba (DNA) kimetoka na kumaliza ubishi kwamba mtoto huyo aitwaye Curtis ni damu halisi ya msanii huyo.
Hivi karibuni, Nay na Siwema ambao walikuwa wapenzi kisha kumwagana, waligombana na kila mmoja kuzungumza lake juu ya mtoto wao huyo ambapo Siwema alidai si damu ya Nay wakati msanii huyo alisema ni damu yake.
Licha ya kupokea majibu hayo mazuri kwake, Nay aliyachukua majibu hayo kwa kuangua kilio cha furaha huku akieleza ya moyoni kuhusiana na sakata hilo.
“Hili ni swala ambalo lilikuwa linaniumiza kichwa kila kukicha. Unajua kama mwanaume, mtu akwambie mtoto si wako unadhani ni maumivu kiasi gani utayapata? Inauma sana, mtu umelea kuanzia mimba hadi mtoto amezaliwa, si kitu kidogo.

“Namshukuru Mungu kwa majibu kwamba ni damu yangu. Mashabiki wangu watambue tu kwamba, Curtis ni mwanangu asilimia mia hivyo hakuna ubishi tena.
“Ujue nampenda sana mwanangu na kwa bahati nzuri huyo ndiye mwanangu wa kiume pekee, hivyo sikutaka kuruhusu wazo lolote kutoka kwa mtu mwingine maana hata kama majibu yasingesema kama ni wangu nilikuwa radhi kuishi naye na kumlea bila kujali hilo kwa sababu tu niliamini siku zote ni mali yangu,” alisema Nay.
Nay aliingia kwenye utata huo takriban mwezi mmoja uliopita baada ya kupishana kauli na Siwema ambaye alimfumania akiwa na mwanaume mwingine nyumbani kwake, jijini Mwanza na kuamua kumchukua mtoto kisha kuishi naye jijini Dar kwa msaada wa mama yake mzaz

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...