Ligi hiyo ya Vodacom itaendelea
kutimua vumbi siku ya jumamosi kwa michezo mitatu, mjini Morogoro
wenyeji Polisi Morogoro watawakaribisha Ndanda FC kwenye uwanja
wa
Jamhuri mjini Morogoro.
Jumapili Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania itaendelea kwa maafande wa timu ya Ruvu Shooting
kuwakaribisha maafande wenzao wa Mgambo Shooting katika uwanja wa
Mabatini – Mlandizi, huku jijini Mbeya wenyeji timu ya Prisons FC
wakiwakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar.
No comments:
Post a Comment