MWANANCHI
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima jana alihubiri akiwa katika kiti cha magurudumu na kusema hawezi kuwatupa Mbunge Edward Lowassa na Dk Wilbrod Slaa kwa kuwa ni marafiki zake wa siku nyingi.
Gwajima alisema
kumekuwa uvumi kwamba kuhojiwa kwake na polisi kulitokana na
kuwakaribisha wanasiasa hao kanisani kwake kwa nyakati tofauti na
kuzungumza na waumini wake.
Askofu huyo amesema alifahamiana na Lowassa tangu mwaka 1996 na alifahamiana na Dk Slaa tangu mwaka 1994 kabla hajagombea nafasi ya Urais kupitia CHADEMA, baada ya hapo urafiki wao walikuwa kama familia.
“Hawawezi
kunichagulia marafiki, hawa ni watu wangu wa karibu hata kabla hawajawa
na ndoto za kugombea urais, nitaendelea kuwa nao karibu,”—Askofu Gwajima.
“Polisi
walinihoji mambo mengi binafsi yanayonihusu mimi na hayakuhusiana
kabisa na Pengo, maswali ya Pengo yalikuwa machache sana,”—Askofu Gwajima.
Hata hivyo, Gwajima alisema hana ugomvi na polisi wala Serikali kwa kuwa amekuwa akitoa ushirikiano kwa vyombo hivyo.
NIPASHE
Askari wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, PC Charles
amejiua kwa kujipiga risasi, baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na
kituo hicho cha polisi walisema tukio hilo lilitokea Aprili 4 mwaka huu
saa 1:00 usiku kituoni hapo.
“Suala
hili limetushangaza, kwani sisi tulikuwa nyumbani. Ghafla tulisikia
mlio wa bunduki katika kituo cha polisi. Tulipofika, tulimkuta askari
huyo akiwa amekufa kwa kujipiga risasi,” alisema Lazaro ambaye ni moja wa mashuhuda.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suzana Kaganda alithibitisha kujiua kwa askari huyo; “Ni kweli askari huyo amejiua kwa kujipiga risasi wakati akiwa kituoni majira ya saa 1:00 usiku,” alisema Kamanda Kaganda.
Kamanda huyo alisema hakuna ujumbe
wowote ulioachwa na askari huyo kuelezea sababu za kujiua na kuwataka
askari wote kutatua matatizo yao kupitia viongozi wao badala ya
kujichukulia sheria mkononi.
Alisema uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha askari huyo kujiua.
MWANANCHI
Mtoto Abdul Mohamedi
ambaye ni mlemavu wa viungo, amelazimika kuishi darini kwa miezi minne
mfululizo kukwepa kudhuriwa na mafuriko kutokana mvua kubwa
zinazoendelea kunyesha Mtwara.
Bibi wa mtoto huyo Zainabu Lipuga alisema jana kuwa alimpandisha darini mjukuu wake Novemba mwaka jana baada ya mafuriko yaliyotekea kipindi hicho.
“Nilipoona
mvua zinanyesha nikaona bora nimnusuru mjukuu wangu asisombwe na
mafuriko kwa vile sina nguvu za kuweza kumpandisha na kumteremsha mara
kwa mara,” alisema Lipuga
Bibi huyo amesema baba wa mtoto hajulikani alipo na jukumu la kumlea limeachwa mikononi mwake bila msaada.
Zaidi ya nyumba 200 zilizingirwa na maji
kutokana na mvua kusababisha hasara kwa wananchi ikiwemo kuharibika
mali zao zikiwamo nguo na vyakula.
No comments:
Post a Comment