KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho
amekiri wazi kupingana na........ tuzo ya Ballon d’Or na anaamini mpira wa
miguu unapoteza muelekeo kwani mafanikio ya timu hayaangaliwi tena.
Cristiano Ronaldo na Lionel
Messi wametawala tuzo hiyo kutoka mwaka 2008, na mwezi januari mwaka huu
mshambuliaji huyo wa Real Madrid na Ureno alishinda tuzo hiyo kwa mwaka
wa pili mfululizo baada ya kufunga magoli 52 katika mechi 43 mwaka
2014.
Arsene Wenger mwanzoni aliweka
wazi kwamba “Hakubaliani kabisa’ na Ballon d’Or kwasabau yeye mapenzi
yake yapo kwenye timu kuliko mchezaji mmoja.
“Nadhani Wenger aliongea kitu
sahihi, anapingana na Ballon d’Or, nadhani yuko sahihi kwasababu kwasasa
mpira umeondoka katika dhana ya timu na kuangalia zaidi wachezaji
binafsi,” Mourinho amesema katika mahojiano maalumu na gazeti la Dail
Telegraph.
“Mara zote tunaangalia takwimu
za mchezaji binafsi, mchezaji anayekimbia sana. Kwasababu umekimbia
kilomita 11 katika mechi nami nimekimbia kilomita 9, wewe wa 11 unakuwa
umefanya kazi nzuri kuliko mimi? labda hapana, labada kilomita 9
zilikuwa muhimu zaidi kuliko 11″.
No comments:
Post a Comment