09 April, 2015

BAADA ya kulazimishwa sare nyumbani dhidi ya Malawi, Tanzania imeporoka kwa nafasi saba

ulimwengu
ZURICH, Uswisi
‘Mwezi uliopita Tanzania ilipanda kwa nafafasi saba kutoka 107 hadi 100, lakini imerejea tena katika nafasi hiyo ya chini.’
BAADA ya kulazimishwa sare nyumbani dhidi ya Malawi, Tanzania imeporoka kwa nafasi saba katika viwango vya kila mwezi vya ubora wa soka vilivyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) leo.

Tanzania (Taifa Stars) iliyolazimishwa sare ya 1-1 nyumbani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wiki juzi, imeporoka kutoka nafasi ya 100 hadi 107 katika viwango vya ubora vya FIFA ikikamata nafasi ya tatu Afrika Mashariki na ya 30 barani Afrika.
Uganda iliyopanda kwa nafasi mbili, inaendelea kuongoza Afrika Mashariki ikiwa nafsi ya 19 barani Afrika na ya 72 duniani ikifuatwa na Rwanda (20, 74), Tanzania, Kenya (34,117) na Burundi 38, 123).
10 bora barani Afrika inaendelea kuongozwa na Algeria wanaokamata nafasi ya 21 duniani ikifuatwa na Ivory Coast (23), Ghana (26), Tunisia (30), Senegal (36), Cape Verde (37), Guinea (41), Nigeria (45), Cameroon (48) na Congo (49).
Mabingwa wa dunia, Ujerumani wanaendelea kuongoza 10 bora duniani wakifuatwa na wanafainali wa michuano ya iliyopita ya fainali za Kombe la Dunia, Argentina, Ubelgiji, Colombia, Brazil, Uholanzi, Ureno, Uruguay, Uswisi na Hispania ambayo wamerejea baada ya kuporomoka mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...