17 April, 2015

Kanye West azindua biblia yake


Hujulikana sana kwa maringo yake,lakini kwa kweli Kanye West asingekufuru na kujitambulisha kama mungu katika biblia hiyo.
Kitabu hicho kitukufu kimebadilishwa na kuwa Biblia ya sasa kwa jina ''Yeezus'' na amini usiamini kila neno la Mungu katika kitabu hicho limeondolewa na
badala yake msanii huyo wa muziki wa kufoka foka ameweka jina lake.
Kulingana na gazeti la The Independence nchini Uingereza,kitabu hicho kinasema kuwa katika kizazi hiki ,Kanye West ndio mkubwa na vilevile kiongozi wa kidini
Kitabu hicho kinaongezea kwamba ''katika utangulizi wetu tunamsherehekea Kanye West na vile alivyotufanyia katika maisha yetu''
Ijapokuwa Kanye hajatoa tamko lolote kuhusu wadhfa huo aliojipatia,amekuwa akijifananisha na Mungu hapo mbeleni.
''Mungu alinichagua mie,alinitengezea njia.Mimi ni chombo cha mungu'',alisema mwaka 2009.
''Lakini kinachoniudhi maishani mwangu ni kwamba sitawahi kujiona nikicheza muziki moja kwa moja''.,aliongezea.
Wasanii wengine waliofananishwa na Yeezy ni Marilyn Monroe na Michael Jackson.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...