JE, PEP Guardiola ndiye kocha bora zaidi duniani?
Ilikuwa wikiendi nzuri kwa
Bayern Munich jana jumapili baada ya Borussia Monchengladbach kushinda
1-0 dhidi ya Wolfsburg na kuwapa ubingwa rasmi The Bavarians.
Kama ilivyoripotiwa na @Squawka,
Pep Guardiola sasa ameshinda mataji matano kati ya 6 aliyoshiriki akiwa
kocha: Matatu na Barcelona na mawili akiwa na timu yake ya Bayern.
@MisterChiping ameeleza
mwanzo mzuri wa Pep: Pep Guardiola ameshinda makombe 19 katika mechi
348 alizoongoza timu ( mechi 247 akiwa na Barca na mechi 101 akiwa na
Bayern), na hii inamaanisha kwamba Mhispania huyo ameshinda taji kila
baada ya mechi 18.
Ukweli mwingine wa Takwimu:
Guardiola ameshinda idadi ya makombe (19) katika miaka 7 sawa na
alivyofanya kocha wa sasa wa Man United Louis van Gaal aliyeshinda idadi
hiyo kwa miaka 24 ya ukocha wake na Sven Goran Eriksson aliyeshinda
idadi hiyo hiyo ndani ya miaka 35 ya kufundisha soka.
Mwisho, Guardiola ameshinda
makombe 19 kati ya 27 aliyoshindania katika maisha yake ya kufundisha
soka na kumfanya awe na mafanikio ya asilimia 70.
Bado rekodi ya Pep inaweza kuongezeaka kwasababu ana uwezekano wa kushinda makombe mpaka 21 kati ya 29.
No comments:
Post a Comment