27 April, 2015

Hazard Mchezaji bora England..

7__eden_hazard___wallpaper_by_aa_designs-d6qocih
Ligi kuu ya England inakaribia ukingoni, na tayari timu mbalimbali zimeshapata taswira kamili ya nini zimepanda kwa msimu mzima wa ligi hiyo ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa.
Chelsea bado ina matumaini makubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo na
wiki ijayo inaweza kutangaza ubingwa endapo itaifunga Crystal Palace baada ya jana kutoka sare ya 0-0 na vibonde wa Arsenal.. Mpaka sasa Chelsea ndiyo inayoongoza kwenye msimamo wa ligi ikiwa na jumla ya pointi zake 77 mkononi.hazardStori ambayo ipo kwenye headlines kwa sasa ni kuhusu kiungo wa ChelseaEden Hazard ambaye amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka na chama cha wachezaji wa kulipwa England, PFA.players
Mchezaji huyo nyota raia wa Ubelgiji ameifungia Chelsea jumla ya mabao 18 akiiwezesha kutwaa taji la kombe la ligi maarufu Capital One pamoja na kuwa mmoja ya wapambanaji waliosukuma jahazi la Chelsea kuelekea kwenye jukwaa la ubingwa kwa mara nyingine tangu mwaka 2010.
Hazard amekabidhiwa zawadi hiyo katika hotel ya Grosvenor Hotel iliyopo London.
Kwa upande wa mwanasoka bora chipukizi mshambuliaji hatari wa SpursHarry Kane alifanikiwa kushinda nafasi hiyo baada ya kuwapiku kipa David De Gea wa Man United na Raheem Sterling wa Liverpool.
_82583402_edenhazard_1
Hii ni record ya Hazard
Tuzo ya heshima ilikwenda na Steven Gerrard na Frank Lampard kutokana na mchango wao mkubwa kwenye ligi kuu ya England.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...