23 April, 2015

Hernandez alifunga goli dakika za mwisho

javier-hernandez-real-madrid_3293878
Hernandez alifunga goli dakika za mwisho kabisa na kupoteza matumaini ya wachezaji pungufu wa Atletico Madrid na kuipeleka timu hiyo anayochezea kwa mkopo nusu fainali,
Mshambuliaji huyo alipata nafasi nzuri na ya wazi dakika ya 88 na kuitumia vizuri na
kupeleka kilio kwa majirani zao hao toka pale jiji la Madrid.
Mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo alikataliwa nafasi mbili za wazi kabla ya kipindi cha kwanza kuisha na kipa imara kabisa wa Atletico Madrid Jan Oblak,pia chicharito alipoteza nafasi mbili za wazi.
Lakini mkwaju wa dakika za mwisho wa Hernandez ulitosha kabisa kwanza kuvunja uteja baada ya kukutana katika mechi nane baada ya fainali ya mabingwa ulaya mwaka jana,ni ushindi wa kwanza baada ya kupoteza mechi nne na kutoka sare mechi 3 kabla ya jana kuvunja uteja huo.
Real Madrid watajua wapinzani wao wa kucheza nao nusu fainali hapo ijumaa pale nchini Switzerland,ronaldo-crisitano-atletico-real-madrid_3293865
Wenyeji waliingia mchezoni mwanzoni kabisa mwa mchezo kwa kumiliki mpira na kupeana pasi fupifupi na kuwamiliki na kupunguza presha huku beki zao Sergio Ramos na Varane ambao walikichafua sana pale nyuma na kuweza kuhimili presha zote hasa kwa wachezaji wajanja kama Ada Turan.
 James Rodriguez alikuwa ndio funguo muhimu ya ushindi wa wenyeji  na mapema kabisa alitengeneza nafasi mbili nzuri kwa Hernandez  kutoka upande wa kulia, lakini mshambuliaji huyo juhudi zake ziliishia kupiga nyavu ndogo za pembeni Muda mfupi baadaye, James Rodriguez alitengeneza nafasi mbili ambazo Hernandez alimeweka pasi kwa ndani kwa Ronaldo, ambaye alipiga shuti la mita 20 lakini hazikuzaa matunda juhudi zake.
 Pia atletico waliweza kuhimili presha za Real kabla ya kadi nyekundu ya Ada Turani dakika kumi na tatu kabla ya mchezo kuisha na hapo ndo mabadiliko ya mchezo yalipoanzia na kupelekea ushindi huo wa mwishoni kabisa kwa wenyeji hao.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...