23 April, 2015

FLOY MYWETHER HATA AKIPIGWA PAMBANO LIJALO ATALIPWA ZAIDI YA DOLA MILION 180.

floyu
Kama ulikua hujui ni kwamba advance atakayolipwa Manny Pacquiao ni pay ya Messi ya miaka karibu miaka 2 akiwa ndani ya mkataba wake wa sasa. Hizi ni fact nyingine kuhusu moja ya matukio makubwa ya kiuchumi kwenye michezo kwa karne hii.

Najaribu kupitia the logistics behind the Mayweather vs Pacquiao fight,pesa zinazoizunguka boxing ya leo.Kwanza ieleweke the highest paid footballer Messi anakula $27m kwa mwaka
Mwaka jana pekee Floyd Mayweather kapigana fights mbili tu na kaingiza $105m,yaani pesa ya Messi kukipiga mpira kwa level hiyo hiyo ya juu kwa miaka 3.8 yaani miaka 3 na miezi 10.Floyd kaingia ulingoni mara mbili tu yaani rounds 12 x 2 ni 24 rounds.Kila round dakika 3 = 72,so huyu hajakaa hata dakika 90 na kaingiza pesa ya miaka karibu 4 ya Messi
Pambano lao la May 2 sasa!.Hadi Mayweather kakubali hii fight wamepitia majadiliano mazito,ngumu kumshawishi Floyd.So Floyd atakula 60% ya total revenues na Manny atakula 40%.Promoter wa Pacquiao kasema Jumatatu anatuma advance (down payment) ya $50m kwa Pacquiao.Yaani advance tu anakula pay ya Messi ya miaka karibu 2.
Baada ya pambano bila kujali nani kapigwa na nani kapoteza,Pacquiao anakula $120m na Floyd anakula $180m.Floyd anaondoka na pesa ya Messi ya miaka 6 na nusu.Pacquiao anaondoka na pesa ya Messi ya miaka 4 na robo.Hiyo ni fight moja tu kwa mwaka!
Jamaa wameshanenepesha account hivyo,Pacquiao anayekula kidogo kuliko mwenzake,baada ya fight na payment yake itambidi aache kodi chini 30% ambayo ni $36m, So anabaki na $84m yaani akirudi kwao Philippines anasema nimetoka kazini,nimelipwa 160bn za kibongo baada ya makato yote
Boxing daah!
160,000,000,000 tshs!!!
Dakika 36 tu ulingoni???

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...