23 April, 2015

Fabrigas kuzomewa jumapil Emirate?

cc
Hii itakua mara ya kwanza kwa Cesc Fabregas kwenda kwenye uwanja wa Emirates na kucheza against timu yake ya zamani kwenye EPL ambayo ni Arsenal. Jumapili hii kwenye EPL kuna mechi kati ya Chelsea na Arsenal ambapo Cesc Fabregas anatengemewa
kucheza mechi hii.
Kuna uwezekano wa Cesc Fabregas kuzomewa kwenye mechi hii na mashabiki wa Arsenal lakini kocha Arsenal Wenger ana mawazo tofauti. Kocha Wenger amesema kwamba mashabiki wa Arsenal waendelee kumheshimu Cesc Fabregas licha ya kuondoka Arsenal akiwa bado ni mchezaji muhimu. Pia Wenger ameongezea kwamba bado anajilaumu kwa kumruhusu Cesc Fabregas kuondoka Arsenal.
Kama wewe ni shabiki wa Arsenal na ungekua uwanja wa Emirates jumapili hii…ungemzomea au ungekausha?

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...