- David de gea amekua akihusiswa na kuhamia Real Madrid misimu huu utakavyokwisha.
- Manchester united wamempa ofay a paundi 200,000 ili abaki
- Kama atasaini atakua golikipa anaelipwa zaidi duniani
- Louis van Gaal alikubali ijumaa hii kwamba klabu imempa mshahara mkubwa sana.
Hofu inaongezeka pale Old Trafford kama hata ongeza mkataba maana yake atarudi kwao Hispania na kujiunga na real Madrid bure kwa sababu mkataba wake utakua umekwisha msimu ujao.
Mpaka sasa hakuna nafuu yoyote katika maongezi hayo ya kumfanya abaki japo kuwa klabu imempa ofay a kulipwa mshahara mkubwa zaidi.
“Tumempa ofa kubwa sana yenye pesa nyingi” alisema Van Gaal ‘Itachukua muda na hivyo ndio mara nyingi inavyotokea lakini mimi sina mamlaka la yeye mwenyewe ndio mwenye maamuzi ya kukubali au kukataa na mkamuulize yeye mwenyewe kama atasaini au la aliongeza van Gaal
United wamempa mshahara wa paundi 180000 pamoja na marupurupu mengine ya ziada nah ii itamfanya awashinde magolikipa wengine wanaolipwa vizuri kama Joe Hart wa man city,Buffon na Manuel Neuer wa Bayern Munic pamoja na iker Cassilas wa Real Madrid.
Lakini hisia zilizopo sehemu ya kubadilishia nguo pale old Trafford ni kwamba De Gea anaweza kuondoka na kwenda kurithi mikoba ya iker Cassilas pale Santiago Bernebeu
No comments:
Post a Comment