Ofisi
ya Msajili wa Vyama vya
Siasa Nchini imekubali maombi ya chama hicho
huku ikiwataka kurudisha cheti cha usajili wa awali na kupewa cheti
kingine.
Awali ACTL-Wazalendo ilipata usajili kwa jina la ACT-Tanzania na baadae kuomba kulibadili jina hilo.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,
Jaji Francis Mutungi, ameridhika na maelezo yaliyokuwa yametolewa na
uongozi wa chama hicho wa sababu za kuamua kubadili jina la chama hicho
kutoka ACT-Tanzania hadi ACT-Wazalendo.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya habari jana jiijini Dar
es Salaam, Jaji Mutungu alijibu ombi hilo kwa njia ya barua.
Katika
taarifa hiyo inaeleza: "Nikurejeshe kwenye barua yenye kumbukumbua
namba AC-HQ/MSJ/2015 ya Aprili 15, mwaka 2015 ikisomwa sambamba na barua
yangu yenye kumbukumbu namba HA.322/362/20/80 ya Aprili 13, mwaka 2015
kuhusu suala tajwa hapo juu".
Jaji
Mutungi alieleza kuwa, alisoma na kuyatafakari kwa kina maelezo katika
barua ya ACT-Wazalendo, na kwamba ameridhika na maelezo yao kuhusu jina
jipya la chama hicho kwa mujibu wa kanuni ya 7 ya kanuni za usajili wa
vyama vya siasa.
No comments:
Post a Comment