10 March, 2016

Samata kuiongoza Taifa Stars AFCON


Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi cha wa wachezaji 25 kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Chad. Mechi hiyo imeratibiwa kusakatwa tarehe 23 Machi mjini Djamena.
Akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza kikosi hicho, Mkwasa, amewaomba wachezaji aliowaita katika kikosi hicho, kujiweka katika hali nzuri ya mazoezi katika vilabu vyao, kwani hakutakua na muda wa kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo huo wa ugenini.
Wachezaji walioitwa Taifa Stars ni magolikipa Aishi Manula (Azam FC), Ally Mustapha (Young Africans) na Shaban Kado (Mwadui FC), walinzi ni Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani (Young Africans), Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, David Mwantika (Azam FC) na Mohamed Hussein (Simba SC).
Viungo Himdi Mao (Azam FC), Ismail Juma (JKU), Jonas Mkude, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto (Simba SC), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Farid Mussa (Azam FC), Deus Kaseke (Young Africans).
Washambuliaji ni Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), John Bocco (Azam FC), Elias Maguri (Stand United), Jeremia Mgunda (Tanzania Prisons) na Ibrahim Hajibu (Simba SC).

09 March, 2016

Magazeti ya Leo Jumatano ya March 9

Video: Linah- Malkia wa nguvu

Itazame hapa video ya "Malkia wa Nguvu" ambayo ni wimbo maalumu uliotengenezwa maalumu kwa ajili ya siku ya wanawake Dunia ambao umeimbwa na Linah, na video hiyo imetengenezwa na Muongozaji Khalifani. Bonyeza PLAY hapo chini kuusikiliza

Madrid, Wolfsburg zatinga robo fainali

Cristiano Ronaldo fires in an effort at goal during the first-half as the Portuguese star looked to add to his tally of goals so far this season
Timu za Real Madrid na Vfl Wolfsburg zimekua timu za kwanza kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa ulaya.
Real Madrid wakicheza katika dimba lao la Santiago Bernabeu wameibuka na ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya As Roma, mabao ya timu hiyo yakifungwa na Cristiano Ronaldo aliyefunga bao lake la 40 kwa msimu huu, na bao la pili likifungwa na James Rodriguez.


Gent midfielder Sven Kums holds off pressure from Wolfsburg's Ricardo Rodriguez on Tuesday night as his side suffer a 1-0 defeat Nao Wajeruman wa Vfl Wolfsburg wamesonga mbele kwa kuwachapa Kaa Gent kwa bao 1-0 bao lilofungwa na mshambuliaji Andre Schurrle, katika mchezo wa wa kwanza Wolfsburg walishinda kwa mabao 3-2.

08 March, 2016

Rihanna Becomes The Only Artist To Have A #1 Hot 100 Single On 7 Consecutive Studio Albums

Rihanna International superstar Rihanna has added another honor to her musical résumé. The Roc Nation songstress is the only artist in history to score a #1 song on seven straight studio albums.
Billboard points out Rihanna earned the distinction when her latest single “Work” topped the Hot 100 chart. The Drake-assisted record off Anti joins “SOS” from A Girl Like Me, “Umbrella,” “Take a Bow,” & “Disturbia” from Good Girl Gone Bad, “Rude Boy” from Rated R, “What’s My Name?,” “Only Girl (In the World),” & “S&M” from Loud, “We Found Love” from Talk That Talk, and “Diamonds” from Unapologetic.
“Work” also helped Rihanna pass Michael Jackson for the third-most Hot 100 #1’s all-time and tie for fifth place on the list of most Top 10 singles in history. Her 14 career #1 singles also include feature appearances on T.I.’s “Live Your Life” as well as Eminem’s “Love The Way You Lie” and “The Mon

Madrid,Wolfsburg kuingia robo fainali?


Michuano ya klabu bingwa Ulaya itaendelea tena leo kwa michezo miwili kuchezwa ikiwa ni nafasi ya kusaka tiketi ya robo fainali.
Miamba wa soka wa Hispania Real Madrid, watakuwa nyumbani katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu kuwaalika As Roma, ambapo Real Madrid wanashuka dimbani wakiwa na faida ya ushindi wa mabao 2-0 walioupata katika mchezo wa kwanza. Katika dimba la Volkswagen Arena huko Ujerumani VfL Wolfsburg watakipiga na Kaa Gent kutoka ubelgiji,VfL Wolfsburg wapo katika nafasi nzuri kutinga Robo Fainali baada ya kushinda Mechi za Ugenini kwa 3-2. Michezo hii itachezwa saa 4:45 kwa saa za Afrika mashariki, Fainali ya michuano hii zitafanyika Mei 28 katika dimba la San Siro huko Milan Itali.

Yanga kuwakabili African Sport Leo


Ligi kuu ya Tanzania bara itaendelea tena leo kwa mchezo mmoja kuchezwa katika uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam.
Klabu ya Yanga watakuwa wenyeji wa wana Kimanumanu African Sports, mchezo utakaopigwa katika dimba la taifa jijini Dar es salaam, mchezo utakaochezwa saa 10:30 kwa saa za Afrika Mashariki. Yanga wako katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi wakiwa na alama 47 wakiwa wamecheza michezo 20 nyumba ya wapinzani wao Simba walioko kileleni kwa alama 48 wakiwa wamecheza michezo 21. Kikosi hicho cha wanajangwani kimeshinda michezo 14, na kwenda sare michezo mitano huku kikipoteza mchezo mmoja. African sport wao wako katika nafasi ya 15 nafasi moja toka mwisho wakiwa wamecheza michezo 21 wana alama 17.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...