Timu za Real Madrid na Vfl Wolfsburg zimekua timu za kwanza kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa ulaya.
Real
Madrid wakicheza katika dimba lao la Santiago Bernabeu wameibuka na
ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya As Roma, mabao ya timu hiyo yakifungwa na
Cristiano Ronaldo aliyefunga bao lake la 40 kwa msimu huu, na bao la
pili likifungwa na James Rodriguez.Nao Wajeruman wa Vfl Wolfsburg wamesonga mbele kwa kuwachapa Kaa Gent kwa bao 1-0 bao lilofungwa na mshambuliaji Andre Schurrle, katika mchezo wa wa kwanza Wolfsburg walishinda kwa mabao 3-2.
No comments:
Post a Comment