08 March, 2016

Madrid,Wolfsburg kuingia robo fainali?


Michuano ya klabu bingwa Ulaya itaendelea tena leo kwa michezo miwili kuchezwa ikiwa ni nafasi ya kusaka tiketi ya robo fainali.
Miamba wa soka wa Hispania Real Madrid, watakuwa nyumbani katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu kuwaalika As Roma, ambapo Real Madrid wanashuka dimbani wakiwa na faida ya ushindi wa mabao 2-0 walioupata katika mchezo wa kwanza. Katika dimba la Volkswagen Arena huko Ujerumani VfL Wolfsburg watakipiga na Kaa Gent kutoka ubelgiji,VfL Wolfsburg wapo katika nafasi nzuri kutinga Robo Fainali baada ya kushinda Mechi za Ugenini kwa 3-2. Michezo hii itachezwa saa 4:45 kwa saa za Afrika mashariki, Fainali ya michuano hii zitafanyika Mei 28 katika dimba la San Siro huko Milan Itali.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...