29 February, 2016

Is A Kanye West & Migos Collaboration On The Way?

Migos 2Kanye West recently revealed that he plans to drop another album this summer. Kanye’s associate, Ian Connor, posted a video to his Snapchat featuring music that sounded like a unreleased Kanye track that might feature Migos. ‘Ye reportedly has more than 40 songs recorded with everyone from Drake, Kendrick Lamar, Young Thug, and more. Kanye has been reppin’ for ATL rappers lately, as his recent Twitter rant stated that Young Thug and Future need to also be a part of the Grammys. It sounds like you will get to hear some interesting collaborations soon.

Video na Audio : Harmonize Ft Diamond Platnumz - Bado

Kutoka Wasafi Classic Studios pata wimbo mpya kutoka kwa Harmonize akimshirikisha Diamond Platnumz katika wimbo mpya BADO!Pia tazama Video ya wimbo huo hapa

YANGA KUMKOSA CANNAVARO MECHI NA AZAM JUMAMOSI

WAKATI Yanga inaingia kambini leo Pemba, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ hatakuwa tayari kwa mchezo mkali wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Machi 5, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa pia, Taifa Stars amesema kwamba anahitaji mechi tatu nyepesi ili aweze kuwa fiti kwa asilimia miamoja baada ya kupona mumivu yake.
Cannavaro alicheza mechi yake ya kwanza kwa dakika zote 90 Jumatano dhidi ya JKT Mlale baada ya kuwa nje tangu Novemba mwaka jana.
“Bado siko fiti, ila baada ya mechi yangu ya kwanza kucheza dakika zote na kwa jinsi ninavyofanya mazoezi, ninahitaji mechi tatu tu ili niwe fiti zaidi”alisema Cannavaro.
Akizungumzia kuhusu nafasi yake ndani ya timu hiyo Cannavaro alisema ushindani uliopo unawapa changamoto wachezaji wote kujituma zaidi ili kumshawishi kocha awape nafasi lakini kwa upande wake yeye ni mpambanaji na hata wachezaji wenzake wanalijua hilo.
“Tupo mabeki wanne wa kati na mwalimu ndio anajua amtumie nani katika mechi ipi, kwa hivyo mwenye kujituma ndiye atakayepewa nafasi,”alisema. 
Yanga inapanda ndege leo kwenda kisiwani Pemba kesho kwa maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Jumamosi ijayo.
Yanga imesonga mbele, Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afriuka kwa kuitoa kwa jumla ya mabao 3-0 Cercle de Joachim baada ya awali kushinda 1-0 katika mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita Mauritius.
Sasa mabingwa hao watetezi wanarudi kwenye vita ya Ligi Kuu, Machi 5 wakimenyana na washindani wao wakuu katika mbio za taji, Azam FC.
Zote, Yanga na Azam FC zina pointi 46 baada ya kucheza mechi 19 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara – lakini mabingwa watetezi wapo kileleni kwa wastani mzuri wa mabao (GD).
Mchezo wa Jumamosi umebeba taswira halisi ya nani atajiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa msimu huu na timu zote zimewekeza katika maandalizi mazuri ndani na nje ya Uwanja.
Azam FC wanakwenda Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ndege kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation kesho dhidi ya Panone Uwanja wa Ushirika.
Na Jumanne watarudi Dar es Salaam na moja kwa moja kuingia kambini katika hosteli zao za Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.


  Chanzo; BinZubery

Manchester City mabingwa wa Capital One

Man City
Manchester City wameshinda Kombe la Capital One baada ya kuwashinda Liverpool kwenye fainali kupitia mikwaju ya penalti.
Willy Caballero ndiye aliyekuwa shujaa wa Manchester City, akiokoa mikwaju ya Lucas, Philippe Coutinho na Adam Lallana baada ya meneja Manuel Pellegrini kuwa na Imani naye na kumchezesha badala ya kipa nambari wani Joe Hart.
Manchester City walianza kwa kujiweka kifua mbele uwanjani Wembley kupitia bao la Fernandinho baada ya kosa la kipa wa Liverpool Simon Mignolet.
Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Raheem Sterling alipoteza nafasi wazi kabla ya Coutinho kusawazisha dakika za mwisho mwisho.
Mambo yaliisha sare 1-1.
Kwenye mikwaju ya penalti, Fernandinho aligonga mlingoti mkwaju wa kwanza wa City, lakini Jesus Navas na Sergio Aguero walifunga huku Caballero, 34, akiokoa mikwaju ya Liverpool na kutoa fursa kwa Yaya Toure kufungwa mkwaju wa ushindi.
Pellegrini alikuwa amebahatisha sana ikizingatiwa kwamba Caballero hakucheza vyema sana mechi waliyoshindwa 5-1 na Chelsea uwanjani Stamford Bridge raundi ya tano ya Kombe la FA.
Wengi wangetarajia amtumie Hart lakini aliamua kukwama na Caballero, ambaye walifanya kazi naye pamoja alipokuwa meneja Malaga.
Pellegrini ndiye aliyemnunua kipa huyo na kumpeleka Manchester.
Baada ya mechi, meneja wa Liverpool Jurgen Klopp alisema: "Tumevunjwa moyo sana lakini lazima tuinuke na kuendelea. Ni wajinga tu ndio husalia chini na kusubiri wachapwe tena.”
Kwa upande wake, Pellegrini alisema alisikitishwa sana na nafasi ambazo walipoteza muda wa kawaida wa mechi ingawa walicheza vyema muda wa ziada.
“Huu ni wakati muhimu sana kwetu, huwa muhimu sana kushinda kombe ukiwa Wembley."

Orodha ya washindi wa Tuzo za Oscars 2016

Washindi
Hii hapa ni orodha ya washindi wa makala ya 88 ya Tuzo za Oscars waliotangazwa katika hafla kuu jijini Los Angeles. Katika vitengo, washindi bado hawajatangazwa, na wanaongezwa kadiri wanavyotangazwa.

Filamu bora zaidi

The Big Short
Bridge of Spies
Brooklyn
Mad Max: Fury Road
The Martian
The Revenant
Room
Spotlight

Mwigizaji bora wa kiume

Bryan Cranston - Trumbo
Matt Damon - The Martian
Leonardo DiCaprio - The Revenant
Michael Fassbender - Steve Jobs
Eddie Redmayne - The Danish Girl

Mwigizaji bora wa kike

Cate Blanchett - Carol
Brie Larson - Room
Jennifer Lawrence - Joy
Charlotte Rampling - 45 Years
Saoirse Ronan - Brooklyn

Mwigizaji bora msaidizi wa kiume

Mshindi: Mark Rylance - Bridge of SpiesChristian Bale - The Big Short
Tom Hardy - The Revenant
Mark Ruffalo - Spotlight
Sylvester Stallone - Creed

Mwigizaji bora msaidizi wa kike

Mshindi: Alicia Vikander - The Danish GirlJennifer Jason Leigh - The Hateful Eight
Rooney Mara - Carol
Rachel McAdams - Spotlight
Kate Winslet - Steve Jobs

Mwelekezi boraAlicia

Lenny Abrahamson - Room
Alejandro G Inarritu - The Revenant
Tom McCarthy - Spotlight
Adam McKay - The Big Short
George Miller - Mad Max: Fury Road

Filamu bora ya kutokana na kitabu

Mshindi: The Big Short (Adam McKay and Charles Randolph)Brooklyn
Carol
The Martian
Room

Filamu bora ya hadithi asili

Mshindi: Spotlight (Tom McCarthy na Josh Singer)Bridge of Spies
Ex Machina
Inside Out
Straight Outta Compton

Filamu bora ya katuni hai

Mshindi: Inside OutAnomalisa
Boy and the World
Shaun the Sheep Movie
When Marnie Was There

Filamu bora ya lugha ya kigeni

Embrace of the Serpent - Colombia
Mustang - France
Son of Saul - Hungary
Theeb - Jordan
A War - Denmark

Filamu bora fupi ya katuni hai

Mshindi: Bear Story (Gabriel Osorio na Pato Escala)Prologue
Sanjay's Super Team
We Can't Live without Cosmos
World of Tomorrow

Filamu bora ya sinema

Mshindi: The Revenant (Emmanuel Lubezki) Carol
The Hateful Eight
Mad Max: Fury Road
Sicario

Filamu yenye mavazi bora

Mshindi: Mad Max: Fury Road (Jenny Beavan) Carol
Cinderella
The Danish Girl
The Revenant

Filamu bora ya makala

Mshindi: AmyCartel Land
The Look of Silence
What Happened, Miss Simone?
Winter on Fire: Ukraine's Fight for Freedom

Filamu bora ya makala fupi

Mshindi: A Girl in the River: The Price of ForgivenessBody Team 12
Chau, Beyond the Lines
Claude Lanzmann: Spectres of the Shoah
Last Day of Freedom

Filamu iliyohaririwa vyema zaidi

Mshindi: Mad Max: Fury Road (Margaret Sixel) The Big Short
The Revenant
Spotlight
Star Wars: The Force Awakens

Filamu bora zaidi ya kuigizwa moja kwa moja

Ave Maria
Day One
Everything Will Be Okay (Alles Wird Gut)
Shok
Stutterer

Filamu ambayo waigizaji wamepambwa vyema zaidi

Mshindi: Mad Max: Fury Road (Lesley Vanderwalt, Elka Wardega and Damian Martin) The 100-Year-Old Man Who Climbed Out the Window and Disappeared
The Revenant

Filamu yenye midundo bora asili

Bridge of Spies
Carol
The Hateful Eight
Sicario
Star Wars: The Force Awakens

Filamu yenye wimbo bora asilia

Earned It, The Weeknd - Fifty Shades of Grey
Manta Ray, J Ralph & Antony - Racing Extinction
Simple Song #3, Sumi Jo - Youth
Til It Happens To You, Lady Gaga - The Hunting Ground
Writing's On the Wall, Sam Smith - Spectre

Filamu yenye maandalizi bora

Mshindi: Mad Max: Fury Road (Colin Gibson and Lisa Thompson)Bridge of Spies
The Danish Girl
The Martian
The Revenant

Filamu iliyohaririwa sauti vyema

Mshindi: Mad Max: Fury Road (Mark Mangini and David White) The Martian
The Revenant
Sicario
Star Wars: The Force Awakens

Filamu iliyochanganywa sauti vyema

Mshindi: Mad Max: Fury Road (Chris Jenkins, Gregg Rudloff and Ben Osmo) Bridge of Spies
The Martian
The Revenant
Star Wars: The Force Awakens

Filamu yenye picha zilizobuniwa vyema

Mshindi: Ex Machina (Andrew Whitehurst, Paul Norris, Mark Ardington na Sara Bennett) Mad Max: Fury Road
The Martian
The Revenant
Star Wars: The Force Awakens

Magazeti Ya TANZANIA Jumtatu Ya Leo Februari 29

28 February, 2016

Mambo yakufanya wewe kama kijana ili Kufanikiwa katika maisha.

    Wahenga walisema "Hasara roho pesa makaratasi" Ndiyoo huu ni ukweli mtupu. Mimi siyo Mswahili ama mmoja wa hao wahenga ila palipo na udhia sinto acha kupenyeza Rupia. Usishangae kuona maneno ya kale hapa maana ni mwanzo tuu na kwa kuyasema hayo la moyoni limenitoka.
Image result for kijana wa kitanzania   Awali ya yote nikusalimu wewe hapo uliye amua kuchukua muda wako wa thamani ili kuipitia Barua hii, na pia nikupongeze wewe mpenzi msomaji wa MAKALA zangu za kila week, kwa kweli naamini utakua umekua ukijifunza kitu kwa namna moja ama nyingine.
   Leo kama kichwa tajwa hapo juu nitakupatia mambo ambayo wewe kama kijana utapaswa kufanya ili ufanikiwa katika maisha.

               1. Jitambue wewe ni nani
    Yawezekana kabisa kufeli kwa mambo yako ni kuto kujielewa wewe ni nani na unapaswa kufanya nini. Vijana wengi wamekua wakiishi tuu pasipo kujitambua wao ni wakina nani na wanapaswa kufanya nini katika wakati gani. Naposema JITAMBUE WEWE NI NANI, simaanishi kua hujijui kua wewe ni wa jinsia gani ama jina lako ni nani, namaanisha Kujitambua kua una  nini na unapaswa kufanya nini juu ya hicho kitu ulicho nacho. Labda nikuulize, je zile ndoto zako ulizowahi kuota ukiwa mtoto kua ukiwa mkubwa utafanya nini zilikwenda wapi ama umezifanikisha kama ulivyo wahi kuziota? Jibu la swali hilo ni kwamba asilimia 85% ni kwamba sivyo ilivyo kama walivyodhani ni itakuja kua. Jambo hili lisikupe tabu, chukua muda wako kama kijana kufanya tathmini ya nini ulicho nacho yaani KIPAJI CHAKO, Kisha wekeza katika hilo kwa bidii na kwa hakika utaona mafanikio. Japo utapata vikwazo juu ya hilo hasa katika maswala ya utendaji lakini Akili yako yakipekee ikitumika utafanikisha.

                  2.Jali muda

      Moja kati ya mambo ambayo yanachangia kuanguka katika maswala ya maendeleo ni kutojali muda. Jambo hili limeonekana sana kua ni tatizo kwa vijana tulio wengi ni kupoteza muda, wahenga walisema "Muda ni mali" unaposhindwa kuujali muda wako basi unakua unapoteza mali hiyo ya thamani katika maisha yako. Hivi unajisikiaje unapokua unafanikisha mambo yako kaitka muda mwafaka? mmmh... ni raha sana au sio? wazungu wanakuambia "One step at a time is always the best" . Rai yangu kwako ni Jali muda wako,

               3.Heshimu Maamuzi yako.    
Mara nyingi sisi kama vijana tumekua tukiyumbishwa mno katika maamuzi yetu, na huku kunatokana na kutokujiamini. Unapokua unashindwa kujiamini na kushindwa kuheshimu maamuzi yako basi unakua katika hali mbaya katika maendeleo yako. Ni kwa nini uyumbishwe? Jambo hili limekua likiwakumba vijana wengi wakike, ndio na hii iko wazi, unakuta mtu kaamua kufanya hivi ila baada yakuyumbishwa kidogo basi anabadili maamuzi yake na moja kwa moja anajikuta katika dimbwi la mahangaiko. Kwa kulitambua hilo utaweza kufanikiwa katika maisha yako.   

              4.Weka nia na malengo katika vyanzo  vyako.
Huu ndio msingi mkubwa katika mafanikio yako, unapokua umetia nia thabiti katika kile unachoamini kua ni mafanikio yako basi huna budi kuwekeza katika hilo na kupanga mikakati thabiti juu ya jambo hilo. Malengo ni dira kamili katika maendeleo yako, iwe ni kuichumi ama biashara, hata katika maisha yako ya kawaida, ndio na ndivyo ilivyo. Wazi mpaka hapo?

               5.Tumia fursa ziliyopo
Hapa naongea na wewe kijana uliekaa tuu mtandaoni masaa 24/7 nakushindwa kutumia fursa uliyo nayo ama iliyo karibu na wewe na mwisho wa siku unaanza kulalamika kua maisha magumu na vitu kama hizo, hapo mimi nitakuita "MPUMBAVU" Zipo fursa nyingi mno zilizo tuzunguka ila tatizo tunakomaa na kazi za kuajiriwa maofisini tuuu pasipo kujua kua hata huyo mwenye office hiyo unayotaka kufanya kazi aliiona fursa ndipo akaamua kuwa na office hiyo. Na hili tatizo nmeliona kwa vijana wengi tulio vyuoni. Tumekua tukipata pesa nyingi mno wakati wa masomo yetu lakini tunaishia kufanya anasa na ujinga wa hapa na pale na mwisho tunapohitimu mashomo yetu tunaanza kuzunguka mjini na bahasha yenye vyeti kutafuta kazi, looooooh!
Ngoja nikuambie kitu, yawezekana ukaniona mwehu ila ni ukweli mtupu "Ukiona umeajiriwa jua umeshindwa kujiajiri"  yaani elimu yote uliyo nayo imekua sawa na bure. Badilika kijana 

              6.Punguza au acha kabisa anasa
Wanasema "ujana maji ya moto" ni kweli kabisa ila katika maisha ya dunia ya leo ukiamini usemii huu hakika utapotea moja kwa moja. Kwanza utaanzaje kuendekeza anasa ilhali una shida zimekujaa hadi utosini? ni jambo lakuamua tuu  na wala sii jambo la lazima, ndio sisi ni vijana bhana na damu zetu zinachemka ila akili zetu zitumike katika hilo, siku nyimi wala siingilii uhuru wako lakini tumia uhuru ulio nao vizuri maana utakuja juta uzeeni.

          7. Weka akiba ya faida unayopata na rizika na kile ulicho nacho
Tumekua tukijidanganya kua "baada ya dhiki ni faraja", kakuambia nani?. Tumekua tukijikuta katika starehe baada ya kupata mafanikio nakusahau kesho japo kesho inajitegemea lakini tunapaswa kuifikiria, isingekua hivyo basi tusingekua tunasema Kesho nitafanya hivi ama lile. Kidogo unachokipata kitumie katika minajili iliyo sahihi. Pia ridhika na ulicho nacho acha tamaaa,

        8. Tafuta mpenzi sahihi na mwenye malengo 
   Hapa nimegusa penyewe. Kwa kweli vijana wengi tumekua tukijihusha na mahusiano na pengine tunakua tunajitumbukiza katika mapenzi na watu ambao sio sahihi. Kuna wapenzi wengine ni hasara tuu jamani. Na hii inatokana sisi wenyewe kujiingiza katika mahusiano na watu ambao hawajapevuka kiakili bali wamepevuka tuu miili ( ha ha ha ha haaaaaa) na hii imekumba vijana wengi wa leo, tumekua tukivutiwa na miili ila kiakili na fikra hatuvutiwi navyo na mwisho wa siku tunakua tunajitwika mizigo miiingi na hadi tunaanguka chini kama punda aliechoka kubeba mzigo. 
Yote hayo ya nini? kwa nini usitulie nakutafuta mpenzi mwenye akili na malengo na mwenye uchungu wa kufanikiwa na ukatulia nae? Jitambue kijana.

     Basi ndugu zangu "mbio za sakafuni huishia ukingoni" na "hakuna marefu yasiyo na ncha" Tumeongea mengi mno na yapo mengi mno ambayo hayajaongelewa hapo juu ila tukutane wakati mwingine hapa hapa MTOKAMBALI tutayajadili mengi. Mkumbuke sana Mungu wako katika maisha yako.

Makala hii imeandikwa na ndugu Francis Mawere
MTOKAMBALI inakukaribisha wewe kuwa mwandishi wao: tafadhali tutumie ujumbe kupitia anwani zifuatazo
Email: mtokambali2015@gmail.com
Au piga 0767322193
             

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...