28 February, 2016

Mambo yakufanya wewe kama kijana ili Kufanikiwa katika maisha.

    Wahenga walisema "Hasara roho pesa makaratasi" Ndiyoo huu ni ukweli mtupu. Mimi siyo Mswahili ama mmoja wa hao wahenga ila palipo na udhia sinto acha kupenyeza Rupia. Usishangae kuona maneno ya kale hapa maana ni mwanzo tuu na kwa kuyasema hayo la moyoni limenitoka.
Image result for kijana wa kitanzania   Awali ya yote nikusalimu wewe hapo uliye amua kuchukua muda wako wa thamani ili kuipitia Barua hii, na pia nikupongeze wewe mpenzi msomaji wa MAKALA zangu za kila week, kwa kweli naamini utakua umekua ukijifunza kitu kwa namna moja ama nyingine.
   Leo kama kichwa tajwa hapo juu nitakupatia mambo ambayo wewe kama kijana utapaswa kufanya ili ufanikiwa katika maisha.

               1. Jitambue wewe ni nani
    Yawezekana kabisa kufeli kwa mambo yako ni kuto kujielewa wewe ni nani na unapaswa kufanya nini. Vijana wengi wamekua wakiishi tuu pasipo kujitambua wao ni wakina nani na wanapaswa kufanya nini katika wakati gani. Naposema JITAMBUE WEWE NI NANI, simaanishi kua hujijui kua wewe ni wa jinsia gani ama jina lako ni nani, namaanisha Kujitambua kua una  nini na unapaswa kufanya nini juu ya hicho kitu ulicho nacho. Labda nikuulize, je zile ndoto zako ulizowahi kuota ukiwa mtoto kua ukiwa mkubwa utafanya nini zilikwenda wapi ama umezifanikisha kama ulivyo wahi kuziota? Jibu la swali hilo ni kwamba asilimia 85% ni kwamba sivyo ilivyo kama walivyodhani ni itakuja kua. Jambo hili lisikupe tabu, chukua muda wako kama kijana kufanya tathmini ya nini ulicho nacho yaani KIPAJI CHAKO, Kisha wekeza katika hilo kwa bidii na kwa hakika utaona mafanikio. Japo utapata vikwazo juu ya hilo hasa katika maswala ya utendaji lakini Akili yako yakipekee ikitumika utafanikisha.

                  2.Jali muda

      Moja kati ya mambo ambayo yanachangia kuanguka katika maswala ya maendeleo ni kutojali muda. Jambo hili limeonekana sana kua ni tatizo kwa vijana tulio wengi ni kupoteza muda, wahenga walisema "Muda ni mali" unaposhindwa kuujali muda wako basi unakua unapoteza mali hiyo ya thamani katika maisha yako. Hivi unajisikiaje unapokua unafanikisha mambo yako kaitka muda mwafaka? mmmh... ni raha sana au sio? wazungu wanakuambia "One step at a time is always the best" . Rai yangu kwako ni Jali muda wako,

               3.Heshimu Maamuzi yako.    
Mara nyingi sisi kama vijana tumekua tukiyumbishwa mno katika maamuzi yetu, na huku kunatokana na kutokujiamini. Unapokua unashindwa kujiamini na kushindwa kuheshimu maamuzi yako basi unakua katika hali mbaya katika maendeleo yako. Ni kwa nini uyumbishwe? Jambo hili limekua likiwakumba vijana wengi wakike, ndio na hii iko wazi, unakuta mtu kaamua kufanya hivi ila baada yakuyumbishwa kidogo basi anabadili maamuzi yake na moja kwa moja anajikuta katika dimbwi la mahangaiko. Kwa kulitambua hilo utaweza kufanikiwa katika maisha yako.   

              4.Weka nia na malengo katika vyanzo  vyako.
Huu ndio msingi mkubwa katika mafanikio yako, unapokua umetia nia thabiti katika kile unachoamini kua ni mafanikio yako basi huna budi kuwekeza katika hilo na kupanga mikakati thabiti juu ya jambo hilo. Malengo ni dira kamili katika maendeleo yako, iwe ni kuichumi ama biashara, hata katika maisha yako ya kawaida, ndio na ndivyo ilivyo. Wazi mpaka hapo?

               5.Tumia fursa ziliyopo
Hapa naongea na wewe kijana uliekaa tuu mtandaoni masaa 24/7 nakushindwa kutumia fursa uliyo nayo ama iliyo karibu na wewe na mwisho wa siku unaanza kulalamika kua maisha magumu na vitu kama hizo, hapo mimi nitakuita "MPUMBAVU" Zipo fursa nyingi mno zilizo tuzunguka ila tatizo tunakomaa na kazi za kuajiriwa maofisini tuuu pasipo kujua kua hata huyo mwenye office hiyo unayotaka kufanya kazi aliiona fursa ndipo akaamua kuwa na office hiyo. Na hili tatizo nmeliona kwa vijana wengi tulio vyuoni. Tumekua tukipata pesa nyingi mno wakati wa masomo yetu lakini tunaishia kufanya anasa na ujinga wa hapa na pale na mwisho tunapohitimu mashomo yetu tunaanza kuzunguka mjini na bahasha yenye vyeti kutafuta kazi, looooooh!
Ngoja nikuambie kitu, yawezekana ukaniona mwehu ila ni ukweli mtupu "Ukiona umeajiriwa jua umeshindwa kujiajiri"  yaani elimu yote uliyo nayo imekua sawa na bure. Badilika kijana 

              6.Punguza au acha kabisa anasa
Wanasema "ujana maji ya moto" ni kweli kabisa ila katika maisha ya dunia ya leo ukiamini usemii huu hakika utapotea moja kwa moja. Kwanza utaanzaje kuendekeza anasa ilhali una shida zimekujaa hadi utosini? ni jambo lakuamua tuu  na wala sii jambo la lazima, ndio sisi ni vijana bhana na damu zetu zinachemka ila akili zetu zitumike katika hilo, siku nyimi wala siingilii uhuru wako lakini tumia uhuru ulio nao vizuri maana utakuja juta uzeeni.

          7. Weka akiba ya faida unayopata na rizika na kile ulicho nacho
Tumekua tukijidanganya kua "baada ya dhiki ni faraja", kakuambia nani?. Tumekua tukijikuta katika starehe baada ya kupata mafanikio nakusahau kesho japo kesho inajitegemea lakini tunapaswa kuifikiria, isingekua hivyo basi tusingekua tunasema Kesho nitafanya hivi ama lile. Kidogo unachokipata kitumie katika minajili iliyo sahihi. Pia ridhika na ulicho nacho acha tamaaa,

        8. Tafuta mpenzi sahihi na mwenye malengo 
   Hapa nimegusa penyewe. Kwa kweli vijana wengi tumekua tukijihusha na mahusiano na pengine tunakua tunajitumbukiza katika mapenzi na watu ambao sio sahihi. Kuna wapenzi wengine ni hasara tuu jamani. Na hii inatokana sisi wenyewe kujiingiza katika mahusiano na watu ambao hawajapevuka kiakili bali wamepevuka tuu miili ( ha ha ha ha haaaaaa) na hii imekumba vijana wengi wa leo, tumekua tukivutiwa na miili ila kiakili na fikra hatuvutiwi navyo na mwisho wa siku tunakua tunajitwika mizigo miiingi na hadi tunaanguka chini kama punda aliechoka kubeba mzigo. 
Yote hayo ya nini? kwa nini usitulie nakutafuta mpenzi mwenye akili na malengo na mwenye uchungu wa kufanikiwa na ukatulia nae? Jitambue kijana.

     Basi ndugu zangu "mbio za sakafuni huishia ukingoni" na "hakuna marefu yasiyo na ncha" Tumeongea mengi mno na yapo mengi mno ambayo hayajaongelewa hapo juu ila tukutane wakati mwingine hapa hapa MTOKAMBALI tutayajadili mengi. Mkumbuke sana Mungu wako katika maisha yako.

Makala hii imeandikwa na ndugu Francis Mawere
MTOKAMBALI inakukaribisha wewe kuwa mwandishi wao: tafadhali tutumie ujumbe kupitia anwani zifuatazo
Email: mtokambali2015@gmail.com
Au piga 0767322193
             

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...