WAKATI
Yanga inaingia kambini leo Pemba, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’
hatakuwa tayari kwa mchezo mkali wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
dhidi ya Azam FC Machi 5, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Nahodha
huyo wa zamani wa timu ya taifa pia, Taifa Stars amesema kwamba
anahitaji mechi tatu nyepesi ili aweze kuwa fiti kwa asilimia miamoja
baada ya kupona mumivu yake.
Cannavaro
alicheza mechi yake ya kwanza kwa dakika zote 90 Jumatano dhidi ya JKT
Mlale baada ya kuwa nje tangu Novemba mwaka jana.“Bado
siko fiti, ila baada ya mechi yangu ya kwanza kucheza dakika zote na
kwa jinsi ninavyofanya mazoezi, ninahitaji mechi tatu tu ili niwe fiti
zaidi”alisema Cannavaro.
Akizungumzia
kuhusu nafasi yake ndani ya timu hiyo Cannavaro alisema ushindani
uliopo unawapa changamoto wachezaji wote kujituma zaidi ili kumshawishi
kocha awape nafasi lakini kwa upande wake yeye ni mpambanaji na hata
wachezaji wenzake wanalijua hilo.
“Tupo
mabeki wanne wa kati na mwalimu ndio anajua amtumie nani katika mechi
ipi, kwa hivyo mwenye kujituma ndiye atakayepewa nafasi,”alisema.
Yanga
inapanda ndege leo kwenda kisiwani Pemba kesho kwa maandalizi ya mchezo
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Jumamosi ijayo.
Yanga
imesonga mbele, Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afriuka kwa kuitoa
kwa jumla ya mabao 3-0 Cercle de Joachim baada ya awali kushinda 1-0
katika mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita Mauritius.
Sasa
mabingwa hao watetezi wanarudi kwenye vita ya Ligi Kuu, Machi 5
wakimenyana na washindani wao wakuu katika mbio za taji, Azam FC.
Zote,
Yanga na Azam FC zina pointi 46 baada ya kucheza mechi 19 za Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara – lakini mabingwa watetezi wapo kileleni kwa
wastani mzuri wa mabao (GD).
Mchezo
wa Jumamosi umebeba taswira halisi ya nani atajiweka kwenye nafasi
nzuri ya kutwaa ubingwa wa msimu huu na timu zote zimewekeza katika
maandalizi mazuri ndani na nje ya Uwanja.
Azam
FC wanakwenda Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ndege kucheza mchezo wa
Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam
Sports Federation kesho dhidi ya Panone Uwanja wa Ushirika.
Na Jumanne watarudi Dar es Salaam na moja kwa moja kuingia kambini katika hosteli zao za Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Chanzo; BinZubery
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment