03 February, 2016

Kampuni ya kurekodi ya Jay Z's Roc Nation, imemshtaki mwanamuziki Rita Ora


Kampuni ya kurekodi ya Jay Z's Roc Nation, imemshtaki mwanamuziki Rita Ora ikidai alivunja kandarasi yake mbali na kutotengeza idadi ya albamu alizoahidi.
Kesi hiyo imeanzishwa mjini New York wiki sita baada ya Rita kuanzisha mashtaka dhidi ya kampuni hiyo mjini Los Angeles.
Rita anadai kwamba kampuni hiyo ina kandarasi haramu naye na kwamba anaomba kutoka.
Rita Ora alijiunga na kampuni hiyo akiwa na umri wa miaka 18 na alikuwa miongoni mwa wanamuziki wa kwanza kusajiliwa na Jay Z.
Tangu ajiunge na kampuni hiyo ya kurekodi muziki ,Rita ametoa albamu moja ya kibinafsi ambayo ni yake ya kwanza mwaka 2012.
Hatahivyo kampuni ya Roc Nation imesema itataka kulipwa dola milioni 2.4 ikisema kuwa imetumia zaidi ya dola milioni 2 kutengeneza na kuiuza albamu ya pili ya mwanamuziki huyo ambayo haijatoka.
Kulingana na ukurasa wa sita wa gazeti la The New York Post,kampuni hiyo inadai kwamba mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 25 aliingia katika kandarasi ya kutoa albamu tano na kampuni hiyo lakini ametoa albamu moja kufikia sasa.
Roc Nation inasema kuwa ilimsajili Rita Ora alipokuwa hajulikani na imemuuzia kazi yake na kuwekeza mamilioni ya madola za kurekodi na gharama nyengine hivyobasi kumsaidia Bi. Ora kupata ufanisi na kuwa maarufu .Wakili wa mwanamuziki huyo ,Howard King,alisema:Jay Z binafsi amemuahidi Rita kwamba atamwachilia huru kutoka katika Roc Nation,maelezo ambayo yanaendelea kufanikishwa

Mikwaju ya penalti ndiyo itakayoamua nani ataingia fainali mechi ya CHAN kati ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo na Guinea.

DR Congo
Timu hizo zilitoshana nguvu muda wa kawaida na mechi ikaingia muda wa ziada uwanjani Amahoro, Uganda.
Ni katika muda wa ziada ambapo Jonathan Bolingi Mpangi kunako dakika ya 101 alifanikiwa kutikiza lango la Guinea.
Lakini katika tukio la kushangaza, mchezani wa Guinea Ibrahim Sory Sankhon amesawazidha dakika ya mwisho ya muda wa ziada.
Mapema kwenye mechi, mchezaji wa DR Congo Padou Bompunga alipewa kadi ya njano dakika ya 38. Hili lina maana kwamba hataweza kucheza fainali iwapo timu yake itafuzu.
Kipa wa DR Congo Ley Matampi pia alipewa kadi ya njano, kosa lake likiwa kunawa mpira nje ya eneo lake.
Rais wa Rwanda Paul Kagame ni miongoni mwa wageni mashuhuri wanaohudhuria mechi hiyo.
Nusufainali hiyo nyingine itachezwa kesho Alhamisi kati ya Ivory Coast na Mali.Kikosi cha DR Congo:
  • Ley Matampi
  • Joyce Lomalisa
  • Padou Bompunga
  • Mechak Elia
  • Doxa Gikanji
  • Christian Ngudikama
  • Nelson Munganga
  • Merveille Bope
  • Joel Kimwaki (Nahodha)
  • Jonathan Bolingi Mpangi
  • Yannick Bangala
Kikosi cha Guinea:
  • Abdoul Aziz Keita (nahodha)
  • Mohamed Thiam
  • Ibrahima Sory Bangoura
  • Alseny Bangoura
  • Ibrahim Sory Sankhon
  • Ibrahima Sory Soumah
  • Moussa Diawara
  • Jean Mouste
  • Alseny Camara
  • Mohamed Youla
  • Aboubacar Leo Camara

FAHAMU NI KWA NINI GIGGS KUTOKUWEPO UWANJANI, MAN UTD vs STOKE YAJULIKANA

Manchester United manager Louis van Gaal takes his seat next to his assistant Ryan Giggs, during a pre season friendly at Old Trafford, Manchester.
Ryan Giggs jana alishindwa kushuhudia ushindi wa timu yake wa bao 3-0 dhidi ya Stoke City katiks uwanja wa nyumbani wa Manchester United, Old Trafford kutokana na matatizo ya kifamilia, gazeti la Dail Mail linaripoti kutoka England.
Kocha Louis Van Gaal alitumia muda mwingi wa mechi hiyo kushauriana na makocha wengine wa mazoezi huku kiti cha msaidizi wake Ryan Giggs kikibakia cheupe.
Aidha magoli yaliyofungwa na Jesse Lingard, Anthony Martial na nahodha Wayne Rooney yalitosha kumpa pumzi kocha Louis Van Gaal ambaye anapitia kipindi kigumu zaidi hivi sasa cha maisha yake ya ukocha, Old Trafford.
Matokeo hayo bado yameibakisha Manchester United katika nafasi ya tano nyuma ya Arsenal wanaoshika nafasi ya nne. Matokeo hayo yanaipa wakati mzuri Manchester United inayotarajia kuivaa Chelsea siku ya Jumapili, Stamford Bridge.

Kisa nadra cha Zika charipotiwa Marekani

Zika
Kisa nadra sana cha virusi vya Zika kuambukizwa kupitia kushiriki ngono, badala ya kuumwa na mbu, kimeripotiwa nchini Marekani.
Mgonjwa aliyeambukizwa virusi hivyo Dallas, Texas, sana huenda aliambukizwa kupitia kufanya mapenzi, Kituo cha Udhibiti wa Maradhi (CDC) kimeambia BBC.
Mtu huyo hakuwa amesafiri maeneo ambayo yana virusi hivyo lakini mpenzi wake alirejea majuzi kutoka Venezuela.
Virusi vya Zika vinaenezwa sana na mbu na vimehusishwa na visa vya watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo na ubongo kudumaa.
Vinaenea kwa kazi Amerika na Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza hali ya tahadhari duniani.Zika
Shirika la msalaba mwekundu nchini Marekani limewahimisha watu waliotoka maeneo yaliyoathirika na Zika, na ambao wanataka kutoa damu, wasubiri angalau siku 28, kabla ya kutoa damu.
Ushauri huu umeelekezwa kwa watu waliorejea Marekani kutoka Mexico, visiwa vya Caribbean au Amerika ya Kati na Kusini katika kipindi cha wiki nne zilizopita, shirika hilo limesema kupitia taarifa.
Katika tukio jingine, visa viwili vya maambukizi ya Zika vimethibitishwa Australia.
Maafisa wanasema wakazi wawili wa Sydey waliopatikana na virusi hivyo walirejea kutoka Caribbean majuzi.
Kisa hicho cha maambukizi ya Zika Dllas, kitakuwa ndicho cha kwanza kuthibitishwa kutokea Marekani bara, ingawa jimbo la Texas limeripoti visa vingine ssaba, vyote kwenye watu waliorejea kutoka nje.
Anne Schuchat, naibu mkurugenzi mkuu wa CDC amesema hicho ndicho kisa cha kwanza kinachohusisha mtu ambaye hakusafiri.
"Hatudhani aliambukizwa baada ya kuumwa na mbu, lakini tunaamini aliambukizwa kupitia kushiriki ngono.”
Taarifa ya CDC imesema njia bora zaidi ya kujikinga na “kujikinga usiumwe na mbu na kutokumbana na manii kutoka kwa mtu aliyekumbana na virusi vya Zika”.
Kisa hicho hata hivyo sicho cha kwanza kabisa cha maambukizi kupitia ngono kuripotiwa.
Shirika la CDC linasema kwenye tovuti yake kwamba mwaka 2013 kulilipotiwa kisa cha maambukizi kupitia kushiriki mapenzi katika jimbo la French Polynesia.
Shirika hilo linawashauri wanawake wajawazito kutosafiri mataifa mengi yaliyoathiriwa sana na virusi hivyo.

CHANZO: BBC

Bondia Amir khan kuzipiga na Sauli Alvarez


Bondia mwingereza Amir khan anatarajia kupigana na bondia kutoka Mexico sauli Alvarez kuwania mkanda wa WBC katika uzito wa kati mnamo mei saba mjini Las Vegas.
Khan mwenye miaka 29, ambaye ni bingwa wa dunia katika uzito wa welter hajapigana tangu apigwe na Chris Algieri mjini New York mwezi Mei.
Kwa upande wake Alvarez mwenye miaka 25, amewahi kumpiga bondia Miguel Cotto kwa pointi mjini Las Vegas mwezi Novemba.
Mpaka sasa amepoteza pambano mara moja huku akishinda mara 46 katika mapambano yake.

Matokeo na msimamo wa Ligi Kuu Uingereza baada ya mechi za February 2


Matokeo ya mechi za Ligi Kuu Uingereza February 2
  •  Arsenal 0 – 0 Southampton
  • Leicester City 2 – 0 Liverpool
  • Norwich City 0 – 3 Tottenham Hotspur
  • Sunderland 0 – 1 Manchester City
  • West Ham United 2 – 0 Aston Villa
  • Crystal Palace 1 – 2 AFC Bournemouth
  • Manchester United 3 – 0 Stoke City
  • West Bromwich Albion 1 – 1 Swansea City

    Msimamo wa Ligi Kuu Uingereza ulivyo sasa
    ligi

Magazeti ya leo Feb 3,2016




Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...