Ryan Giggs jana alishindwa kushuhudia ushindi wa timu yake wa bao 3-0 dhidi ya Stoke City katiks uwanja wa nyumbani wa Manchester United, Old Trafford kutokana na matatizo ya kifamilia, gazeti la Dail Mail linaripoti kutoka England.
Kocha Louis Van Gaal alitumia muda mwingi wa mechi hiyo kushauriana na makocha wengine wa mazoezi huku kiti cha msaidizi wake Ryan Giggs kikibakia cheupe.
Aidha magoli yaliyofungwa na Jesse Lingard, Anthony Martial na nahodha Wayne Rooney yalitosha kumpa pumzi kocha Louis Van Gaal ambaye anapitia kipindi kigumu zaidi hivi sasa cha maisha yake ya ukocha, Old Trafford.
Matokeo hayo bado yameibakisha Manchester United katika nafasi ya tano nyuma ya Arsenal wanaoshika nafasi ya nne. Matokeo hayo yanaipa wakati mzuri Manchester United inayotarajia kuivaa Chelsea siku ya Jumapili, Stamford Bridge.
No comments:
Post a Comment