Bondia mwingereza Amir khan
anatarajia kupigana na bondia kutoka Mexico sauli Alvarez kuwania mkanda
wa WBC katika uzito wa kati mnamo mei saba mjini Las Vegas.
Khan
mwenye miaka 29, ambaye ni bingwa wa dunia katika uzito wa welter
hajapigana tangu apigwe na Chris Algieri mjini New York mwezi Mei.Kwa upande wake Alvarez mwenye miaka 25, amewahi kumpiga bondia Miguel Cotto kwa pointi mjini Las Vegas mwezi Novemba.
Mpaka sasa amepoteza pambano mara moja huku akishinda mara 46 katika mapambano yake.
No comments:
Post a Comment