Uingereza itakuwa na Waziri Mkuu mwanamke, ambaye atachukua majukumu kufikia mwezi Oktoba.
Waziri wa mambo ya ndani Theresa May, ndiye anayepigiwa upatu sana kumrithi David Cameron kama kiongozi wa chama na waziri mkuu.
Waziri wa kawi Andrea Leadsom, ndiye mwanamke huyo mwingine.
Waziri wa Haki Michael Gove, aliyekuwa mmoja wa waliopigia debe Uingereza kujitoa Muungano wa Ulaya, alimaliza wa tatu kwenye kura ya akaondolewa.
Matokeo kamili yanatarajiwa mwezi Septemba.
Kinyang’anyiro cha sasa cha kuchagua kiongozi mpya kilianza baada ya Bw Cameron kuamua kung’atuka.
Hii ni baada ya upande wake, uliotaka Uingereza isalie EU, kushindwa kwenye kura ya maoni mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment