Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Damian Lubuva
amewataka wanasiasa walioshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu waache kujitangaza
kuwa walishinda, akisema wanapotosha wananchi.
Kauli hiyo ya Jaji Lubuva imekuja siku chache baada ya aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa kudai kuwa kama si
matokeo kuchakachuliwa, alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda kwa sababu
wananchi walishaichoka CCM na wakawa wanataka mabadiliko.
Lowassa alisema hayo katika mahojiano maalum na waandishi wa habari
ofisini kwake, akisema yeye na Ukawa walishinda kwa kishindo isipokuwa
matokeo yalivurugwa makusudi ili CCM iendelee kubaki madarakani.
Jana, akiwa kwenye mkutano wa tathmini kati ya NEC na asasi za kiraia
kuhusu utoaji elimu kwa mpigakura uliofanyika Dodoma, Jaji Lubuva
alisema uchaguzi umeshapita na kilichobaki sasa ni kufanya kazi tu.
Bila ya kutaja jina la mwanasiasa huyo, Jaji Lubuva alisema kama kuna
mtu alishindwa katika uchaguzi uliopita, ajipange kwa ajili ya uchaguzi
mkuu ujao mwaka 2020.
“Hata wananchi wanawashangaa kwa kuwa wao ndio walioamua ni nani anafaa kuwaongoza,” alisema Jaji Lubuva.
Alisema kuwa NEC ilikuwa inapokea matokeo ya uchaguzi kutoka majimboni
na kuyasoma kama yalivyotumwa na katika hilo hakuna wakala hata mmoja wa
chama ambaye aliyapinga matokeo hayo. “Sasa nashangaa kuna baadhi ya wagombea wanaotaka Tume ifukuzwe kazi eti
tu kwa sababu wao hawakushinda. Naomba ifahamike kwamba katika kila
uchaguzi duniani kuna kushinda na kushindwa.
"Sasa kama kila atakayeshindwa atataka tume ifukuzwe kazi hapatakuwa na
tume ya uchaguzi kwa sababu kila atakayekuwa anashindwa atakuwa anataka
tume ifukuzwe kazi,” alisema Jaji Lubuva.
08 February, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment