Raia wa Switzerland Gianni Infantino amechukua mahala pake Sepp Blatter kama rais wa shirikisho la soka duniani Fifa.
Katibu huyo mkuu wa Fifa alipata
kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya mpinzani wake
wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa.
Mwanamfalme Ali bin al-Hussein alikuwa wa tatu akiwa na kura nne huku Jerome Champagne akishindwa kupata hata kura moja.Tokyo Sexwale alijiondoa kabla ya kura kuanza kupigwa mjini Zurich.
Wingi wowote wa kura[zaidi ya aslimia 50] katika raundi ya pili ya uchaguzi huo ulikuwa unaweza kumwezesha mgombea kutangazwa mshindi katika raundi ya pili.
Infantino ni wakili mwenye umri wa miaka 45 kutoka eneo la Brig jimbo la Valais nchini Switzerland ,ikiwa ni eneo lililopo chini ya maili sita kutoka nyumbani kwa Blatter.
Blatter ambaye aliliongoza shirikisho hilo tangu mwaka 1998 alijiondoa mwaka uliopita kabla ya kupigwa marufuku katika shughuli zozote za kandanda kwa kipindi cha miaka sita.
Lakini aliwaambia wajumbe kwamba ”kwa pamoja wataweza kuirudisha sura ya Fifa na heshima ya Fifa”.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment