Klabu ya Manchester United na
Manchester City watakutana katika roundi ya nne katika kombe la Ligi ya
Uingereza (EPL) uwanjaini Old Trafford.
United waliibuka na
ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Northampton siku ya Jumatano
huku City wakiibuka na mabao mawili kwa moja dhidi ya Swansea.Kwengineko, timu ya West Ham itawakaribisha mahasimu wa Uingereza Chelsea, huku Tottenham wakielekea Liverpool.
Timu zitakazo toka sare zitacheza kuanzia tarehe 24 mwezi Oktoba.
City walishinda kombe hilo msimu uliopita baada ya kuishinda Liverpool kwa mikwaju ya penalti.
United wakiongozwa na Jose Mourinho wamepata ushindi mara tatu mfululizo dhidi ya Northampton.
DROO KAMILI:
West Ham dhidi ya Chelsea
Manchester United dhidi ya Manchester City
Arsenal dhidi ya Reading
Liverpool dhidi ya Tottenham
Bristol City dhidi ya Hull
Leeds dhidi ya Norwich
Newcastle dhidi ya Preston
Southampton dhidi ya Sunderland
No comments:
Post a Comment