Aliko Dangote, mtu tajiri zaidi
barani Afrika,ana mpango wa kuinunua klabu ya Arsenal kutoka nchini
Uingereza katika kipindi cha miaka minne.
Alisema kuwa anasubiri biashara zake kuimarika pamoja na uwekezaji wake wa ujenzi wa bomba la gesi na kiwanda cha kusafisha mafuta kabla ya kukinunua klabu hicho.
''Hakuna tatizo kwamba atakinunua klabu hicho'' na si tatizo la fedha ,alisema Dangote katika mahojiano na runinga ya Bloomberg .
''Pengine miaka mitatau au mine.Swala ni kwamba tunachangamoto nyingi.Ninahitajika kukabiliana nazo mwanzo baadaye nitaangazia swala la ununuzi huo''.
Dangote ambaye ni shabiki mkubwa wa Arsenal amepoteza kiasia cha dola bilioni 4.4 mwaka huu kutokana na kushuka kwa thamani ya sarufi ya Nigeria.
Utajiri wake mwingi upo katika kiwanda cha simiti cha mjini Lagos.
Iwapo atainunua timu hiyo basi atakuwa mtu wa kwanza kutoka barani Afrika kumiliki timu iliopo katika ligi kuu ya Uingereza.
No comments:
Post a Comment