Mtu mmoja na mkewe kutoka jamii ya
Daliti inayobaguliwa tangu jadi nchini India wameuawa, mmoja akiwa
amekatwa kichwa na mwengine kunyongwa kwa kushindwa kulipa deni la Rupee
kumi na tano ambalo ni karibu senti ishirini na mbili tu.
Mfanyi biashara huyo amekamatwa.
Ubaguzi kwa misingi ya kijamii umeenea sana nchini India, huku watu wa jamii ya Daliti waliokuwa wamebadikwa jina la 'the untouchables' wakiwekwa kwenye daraja la chini kabisa kwenye sera hiyo ya kibaguzi nchini India iitwayo 'caste' ambapo wananyimwa fursa nyingi za kimaendeleo na hivyo kubaki katika lindi la umaskini .
Hata hivyo Visa vya ukatili wa kibaguzi dhidi ya jamii ya Dalit katika jimbo la Gujarat vimeongezeka mnamo siku za hivi karibuni na vimesababisha wimbi la maandamano kutoka watu wa jamii hiyo.
No comments:
Post a Comment