31 July, 2016

Tetesi za soka Barani Ulaya..



Arsenal wataongeza dau na kufikia pauni milioni 35 kumtaka mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette, 25, baada ya dau la awali la pauni milioni 29.3 kukataliwa na klabu hiyo ya Ufaransa (Daily Telegraph).

Arsenal pia wanataka kumsajili beki wa Torino, Bruno Peres, 26, huku klabu hiyo ikitaka pauni milioni 16.9 kulingana na (Gazzetta World).
Vilevile klabu hiyo inazungumza na Valencia kutaka kumsajili beki mjerumani Shkodran Mustafi, 24, ambaye ana kipengele cha uhamisho chenye thamani ya pauni milioni 42.1 kwenye mkataba wake (Sky Sports).

Dau la Chelsea la pauni milioni 57, kumtaka mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku, 23, limekatakiwa, huku klabu hiyo ikitaka pauni milioni 75 (Daily Mirror).
Kiungo wa Tottenham Christian Eriksen, 24, amekataa kusaini mkataba mpya, kwa sababu anataka mshahara wake wa pauni 30,000 kwa wiki kuongezwa (Evening Standard).
Nayo Swansea wamepanda dau la kumtaka mshambuliaji wa Sevilla, Fernando Llorente, 31, baada ya Bafetimbi Gomis kwenda Marseille kwa mkopo hadi mwisho wa msimu, na hivyo hawana mshambuliaji rasmi kwa sasa (Daily Mail).

Wakati huohuo Leicester City wako tayari kumpa mkataba wa pauni 100,000 kwa wiki kiungo Riyad Mahrez, 25 ambaye inaaminika anasakwa na Arsenal (Daily Express).
Na hayo yakijiri Manchester United inakaribia kumsajili beki wa kulia kutoka Brazil anayechezea Monaco, Fabinho, 22 (globoesporte).

Aston Villa wanaonekana watamuuza Idrissa Gana, 26, huku Everton wakiwa tayari kukamilisha usajili wa pauni milioni 7.1 kumchukua mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal (Daily Mirror). Vilevile beki wa Manchester United Cameron Borthwick-Jackson, 19, huenda akaondoka Old Trafford na kwenda kucheza kwingineko kwa mkopo (Manchester Evening News).

 
Everton hawajapanda dau lolote kumtaka beki wa Sunderland Lamine Kone, 27, licha ya taarifa kuzagaa kuwa dau la pauni milioni 14 limetolewa (Sunderland Echo).

Everton wanataka kumsajili beki wa Swansea Ashley Williams, 31, ambaye huenda akagharimu pauni milioni 10 kwa mujibu wa (Daily Mirror).
Nayo Manchester City wanasita kutoa pauni milioni 50 kumsajili beki wa kati wa Everton John Stones, 22, wakitaka kutoa takriban pauni milioni 40 (guardian).
Mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino, 22, yuko tayari kubakia katika klabu hiyo hadi mkataba wake utakapomalizika msimu ujao na aondoke kama mchezaji huru (ESPN).
Klabu ya Galatasaray inataka kumsajili beki wa Manchester City Jason Denayer, 21, na pia kiungo wa Liverpool Lucas Leiva, 29 (Daily Mirror). 
Manchester City watathibitisha kuwa Sergio Aguero, 28, atasaini mkataba mpya kabla ya kuanza kwa msimu (Daily Mail).


loading...

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...