Kupitia kipindi cha Power 180 cha Sibuka Fm Chid ameweka wazi kuwa hajajiunga na lebo hiyo bali huwa anashinda kwenye ofisi za label hiyo kwa sababu za kiusalama asije akarudi kwenye matatizo yaliyompata (matumizi ya madawa ya kulevya) na huwa anafanya kazi ndani ya studio hizo inapobidi.
“Sijasaini pale ila ni sehemu ambayo huwa nafanya kazi, na wale ni wadogo zangu kwa hiyo kushinda nao ni wao wanahitaji niwe pale kwa sababu za ki usalama zaidi,ili wajiridhishe kwamba sipo kwenye kona kona zingine,kwa sasa hivi niko hivyo lakini nikiamua hata kesho naweza kuwaambia naombeni karatasi na peni nikafanya hivyo”alisema Chid Benz ambaye hivi karibuni ameachia wimbo wake unaoitwa Chuma.
No comments:
Post a Comment