Refarii wa kike wa kimataifa wa
Tanzania mwenye beji ya FIFA, Jonesia Rukyaa ameteuliwa kuungana na
waamuzi kutoka nchini Kenya kuchezesha mchezo wa kuwania kufuzu kwa
Fainali za Kombe la dunia kwa wanawake wenye umri chini ya miaka 17
(WWC-Q 17) mwishoni mwa mwezi huu.
Jonesia Rukyaa atakua mwamuzi
wa akiba katika mchezo huo kati ya Misri dhidi ya Cameroon utakaochezwa
jijini Cairo wikiendi ya tarehe 25,26,27 Machi, 2016.Muamuzi wa kati katika mchezo huo atakua ni Carolyne Wanjala (Kenya), akisaidiwa na Carolyne Kiles (Kenya), Mary Njoroge (Kenya), huku kamishna wa mchezo huo akiwa ni Leah Annette Dabanga kutoka jamhuri ya Afrika ya Kati.
No comments:
Post a Comment