Mechi za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za Uefa Europa Ligi zinatarajia kuendelea leo Alhamisi kwa michezo miwili.
Manchester
United na Tottenham zote ziko Viwanja vya Nyumbani kwao vikidaiwa
kushinda kwa ushindi wa kishindo ili kutinga Robo Fainali kufuatia
vipigo katika Mechi zao za kwanza.Tottenham, maarufu kama Spurs wako kwao White Hart Lane Jijini London kurudiana na Vigogo wa Germany Borussia Dortmund ambao walishinda Mechi ya kwanza 3-0 na hivyo Spurs wanapaswa kushinda 4-0 ili kusonga.
Nako huko Old Trafford ni marudiano ya Mahasimu wakubwa wa Soka la England ambapo Man United wanatakiwa waifunge Liverpool 3-0 ili wasonge baada ya kutandikwa 2-0 Wiki iliyopita huko Anfield kwa Bao za Penati ya Daniel Sturridge na Roberto Firmino.
No comments:
Post a Comment