Ligi ya mabingwa iliendelea tena hapo jana ambapo kulikua na michezo miwili iliyokua ikichezwa ili kuwania nafasi yakutinga robo fainali na Man City wao walikua wakiumana na Dynamo Kiev ambapo mchezo huo ulitoka suluhu ya bila kfungana na kuifanya Man City kusonga mbele kufuatia kuwa na ushindi wa bao 3-1 walioupata mchezo wa awali.
Rekodi zilizowekwa na Man City
- Manchester City ni timu ya saba nyingine tofauti kuingia robo fainali ya Champions League kutoka England baada ya Arsenal, Tottenham, Leeds, Liverpool, Manchester United pamoja na Chelsea tangu mwaka 1992
- Man City wameweka rekodi ya kucheza mechi 10 bila kuruhusu nyavu zao kutikiswa kwenye michuano hiyo ya Ulaya mara ya mwisho ilikuwa ni December 2014 dhidi ya Roma.
- Mchezo wa jana usiku ulikuwa ni wa pili Manchesyer City inacheza dakika 90 bila kupata bao kwenye michuano ya Champiuons League ndani ya uwanja wa Etihad
- City waliweza kupiga shuti moja tu on target wkati wa mchezo, shuti hilo lilipigwa dakika ya 73 kipindi cha pili.
No comments:
Post a Comment