16 March, 2016

Ligi Kuu ya Tanzania bara kuendelea tena leo

Ligi Kuu ya Tanzania bara inatarajiwa kuendelea leo kwa mchezo mmoja, ambapo Azam FC watawakaribisha Stand United.
Ijumaa mkoani Shinyanga katika uwanja wa Kambarage, wakata miwa wa Kagera Sugar watakua wenyeji wa ndugu zao kutoka wakata miwa Mtibwa Sugar kutoka Manungu Turiani.
Wikiendi Jumamosi na Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa michezo mitano kuchezwa katikwa viwanja mbalimbali nchini, jijini Tanga wenyeji Coastal Union wakiwa wenyeji wa Simba SC katika uwanja wa Mkwakwani jijini humo.
Majimaji FC itakua nyumbani katika uwanja wa Majimaji mjini Songea kucheza na Mbeya City, huku chama la wana Stand United wakiwakaribisha Ndanda FC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.Wachezaji wa Simba wakimlaki Awadh Juma baada ya kufunga bao na kuihakikishia timu yake kupata pointi tatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya TZ Prisons

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...